MASOKO YA BIASHARA YATAKIWA YAWE MASAFI KIBAHA

Julieth Ngarabali,  Kibaha.

 Kuanza kunyesha kwa mvua katika maeneo mbalimbali, Wafanya biashara katika soko la Picha ya ndege mjini Kibaha mkoani Pwani wametakiwa kuchukua tahadhari ya magonjwa ya mlipuko kwa kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.

Picha ikionyesha baadhi ya mifuko ikiwa imetupwa ovyo ovyo venye uchafu ndani yake.


Diwani wa kata hiyo Karim Mtambo amesema maeneo mengi ya soko kuna mabaki ya bidhaa ambayo hayaonekani kama ni taka kiurahisi lakini kutokana na kutirirka maji ya mvua hovyo na muda mrefu mabaki hayo huoza na kusambaa kama uchafu.


Amesema mfano halisi wa mabaki Nn maganda ya kabichi , embe zinazomenywa sokoni, mananasi , mabaki ya mboga za majani ambapo zinapokusanyika pamoja hutengeneza uchafu na hata kutoa harufu inayovuta inzi.


"Sasa huu mchanganyiko huu wasipokua makini unakua uchafu unavuta wadudu kama inzi na hata funza hivyo kuweza kuleta madhara" amesema Mtambo


 Mmoja wa wafanyabiashara wa eneo hilo Jabir Issa ameahidi kushirikiana na wengine kuhakikisha mabaki ya aina hiyo yanatengwa na kutupwa kila siku Kwenye mashimo ya taka au dampo


Pia wameomba gari ya taka la halmashauri liwe linafata kwa wakati taka zilizotupwa kwenye makontena  ili kuepusha Kasi ya maji ya  mvua kuzisambaza sokoni humo au mtaani .


Mwisho

Post a Comment

0 Comments