DATUM YASHUSHA NEEMA CLOUD MEDIA.

Na Shushu Joel. 

KAMPUNI ya uuzaji na upimaji wa viwanja hapa nchini ya Datum  imewakabidhi wafanyakazi wa kampuni ya Cloud Media Group Hati za umiliki wa viwanja watumishi hao katika maeneo ya Buyuni yaliyoko Kigamboni Jijini Dar es Salaam .

Mkurugenzi wa kampuni ya Datum Ezekiel Masanja akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa Cloud Media mara baada ya kuwakabidhi hati za umiliki wa viwanja vyao.(NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza Wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi wa Kampuni hiyo  ya Datum Ezekiel Masanja alisema kuwa kampuni yao imekuwa msaada mkubwa kwa wananchi mbalimbali hapa nchini katika kuhakikisha watu wote wanamiliki Ardhi yao kwa lengo la kujenga nyumba zao.

"Imekuwa ni ngumu kwa wanyonge kuweza kumiliki Ardhi lakini kampuni yenu imekuwa ikifanikisha ndoto za wanyonge  hao kwa kuwafanikishia ndoto zao za umiliki wa maeneo"Alisema Masanja.

Aliongeza kuwa wafanyakazi waliokabidhiwa hati na kuonyeshwa viwanjwa vyao kwa leo ni watu 27 huku wengine wakitakiwa kuendelea kumalizia madeni yao ili nao wakabidhiwe kama walivyokabidhiwa wenzao.

Aidha alisema kuwa Kampuni yao imetengeneza mfumo ambao ni rahisi sana kwa kila mnyonge kwani imeruhusu malipo ya kidogo kidogo mpaka watakapo kamilisha malipo yao.


Hivyo Mkurugenzi huyu amewataka wananchi mbalimbali kuchangamkia fursa zinazopatikana katika kampuni hiyo ya Datum ili kukamilisha usemi wa Baba mwenye nyumba na si ule wa Baba mwenye gari.


Kwa upande wake Mmoja wa wafanyakazi wa Cloud media aliyepata Hati Bw, Elikimbilio Kitoa alisema kuwa ilikuwa ni kama ndoto lakini leo naye anamiliki kiwanja chake tena kigamboni kweli Mungu yupo.


Aliongeza kuwa ni vyema vijana tukawekeza kwenye viwanja na umiliki wa nyumba zetu kwani sehemu ya kulala ni muhimu kuliko sehemu zingine.


Naye Mkuu wa wilaya hiyo  Sara Msafiri ameipongeza kampuni ya Datum kwa jinsi ambavyo imekuwa mkombozi wa wananchi kwa kuuza viwanja kwa kulipa fedha kidogo kidogo .

Aidha alisema kuwa Serikali itaendelea kuwa nae bega kwa bega katika kuhakikisha viwanja walivyonavyo vinauzwa kwa wananchi wanyonge cha msingi ni kufuata kanuni na sheria za ujenzi wa mipango maji.

 Pia alisema kuwa ni wakati wa Kigambani sasa kuonekana kwani tumefungua fursa za wilaya yetu.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments