Harold Shemsanga, Kibaha.
![]() |
| Hii ndio hofu ya wananchi hawa |
Wakazi katika Kijiji cha Lukenge Kata ya Magindu Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani wamesema wapo katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na wengi wao kutumia maji yasiyo safi na salama.
Wananchi hao wametoa kilio hicho kwenye kikao kati ya viongozi wa Vitongoji vinavyounda Kijiji hicho ambacho pia kilihudhuriwa pia na msimamizi mkuu wa usambazaji maji safi kutoka DAWASA Kibaha , Mhand8si Hafidhi Mketo
Akizungumza mmoja wa wakazi hao Daudi Maulid alisema hali katika kijiji hicho si shwali huku akiiomba Halmashauri iboreshe lambo lao hilo ili waendelee kutumia maji safi na salama wakati wakisubiri mradi wa maji ya bomba kutoka DAWASA .
Alisema kuna wakati kunatokea watu wengi wanalalamika kuumwa magonjwa ya matumbo kutokana na matumizi ya maji hayo ambayo yanapatikana kwenye lambo ambalo nalo linatumiwa na mifugo,
"Hapa kijijini pamoja na kuwepo na huduma ya maji, lakini kwa muda mrefu hayajatoka tunalazimika kutumia haya ya kwenye lambo ambayo ndiyo hivyo tena na mifugo kuwa safi na salama, tunaomba uongozi wa halmas hauri utuboreshee lambo letu ," alisema Ramadhan Urembo
Kwa upande wake Michael Lufunga Mwenyekiti wa Kijiji cha Kingule alisema katika kupamabana na changamoto hizo atashirikiana na Diwani wa Kata hiyo Erasto Makala kutoa zawadi kwa mtu yeyote atakaye haribu miundombinu ya maji na kwamba atamzawadia atayemkamata anayehujumu kiundonbinu hiyo.
"Ninawaagiza wakazi katani hapa kuwabaini watu wanaojihusisha na uharibifu wa vyanzo vya maji, ikiwemo ukataji wa mabomba atayefanikisha kupatikana kwa mtu huyo nitamzawadia kitita cha shilingi milioni moja taslimu," alisema Makala.
Akizungumzia mikakati ya DAWASA ya kuwaondolea adha hiyo, Mhandisi Mketo alisema uongozi una mopango mikubwa ya kuondoa kadhia hiyo, huku akieleza kuwa tayari huduma ya maji inapatikana ikilinganishwa na kipindi kilichopita.
Aliongeza kwamba kuna mradi mwingine mkubwa wa Mlandizi Msoga, unaotekelezwa hivi sasa ambao utaweka matenki makubwa yanayolenga kuondoa kabisa kadhia hiyo kwa wananchi katika maeneo ya Gwata, Magindu mpaka Lukenge na vitongoji vyake.
MWISHO.

0 Comments