KIJIJI CHA KWALA CHATENGA ENEO LA KUTUPIA TAKATAKA.

NA HAROLD SHEMSANGA. KIBAHA

Kijiji Cha kwala halmshauri ya Kibaha Vijijini. Umeamua kutenga Eneo ambalo litatumika kuhifadhia taka zinazozalishwa katika Kijiji hicho kwa lengo la kuondoa taka hizo katika makazi ya watu.

Wananchi wa kijiji cha Kwala wakiwa kwenye kikao  kilichoamua kutenga eneo kwa ajili ya kutupia taka taka zao.

Akiongea katika Mkutano wa Kijiji diwani wa Viti Maalumu ambae pia ni mwenyekiti wa Huduma za Jamii halmshauri ya Kibaha Vijijini Josephine gunda amesema kwala Sasa imekuwa na msongamano wa watu umeongezeka hivyo wameona ni vyema kutenga Eneo (Dampo) kwa ajili kupata sehemu itakato tumika kuhifadhia taka hatua itakayo saidia kuondokana na magonjwa ya Mlipuko na hivyo kuhatarisha Afya za wakazi wa Eneo Hilo.


"Ujue kwala imekuwa Sana kutokana na fulsa za uwepo wa miradi mikubwa Kama vile ujenzi wa bandari kavu na ujenzi wa reli umeongeza watu hivyo tumeona ni vyema kujipanga mapema kulinda Afya za wananchi wetu wasije pata magonjwa ya Mlipuko ambayo ni hatari" Alisema Josephine Tunda


Ameongeza kuwa uongozi wa Kijiji Cha kwala umewasilisha ombi katika ofisi ya Aridhi halmshauri ya Wilaya kibaha kufika Kijijini hapo kwa ajili ya kuangalia Eneo lililotengwa na kutoa ushauri Kama lipo Eneo linalokubalika ili Kazi ya kukusanya taka mtaani iweze kuanzia.


Ikumbukwe mwishoni mwa Mwaka Jana Mh Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa aliagiza kata ya kwala kuanza kupangwa katika mpango Bora ambao utaruhusu fulsa zaidi ya kiuwekezaji na kuongeza ajira kwa wakazi.


Akizungumza katika kikao hicho mmoja wa wananchi hapo Said Rajabu amepongeza hatua ya kupatikana kwa Eneo litakalo tumika kuhifadhia taka ili kupunguza mlundikano majumbani na hivyo kujiepusha na magonjwa ya Mlipuko.


Kijiji Cha kwala ni muongoni mwa Vijiji vya siku nyingi lakini kwa katika ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la wananchi hivyo viongozi kuamua kuongeza umakini katika kutunza Mazingira pamoja na usafi.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments