Na Shushu Joel,Mkuranga.
MKUU wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani Filberto Sanga amewataka walimu wote katika wilaya hiyo kuwa mstali wa mbele katika kutunza thamani za shule ili zitumike kwa muda mrefu.
Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akizungumza na walimu wa shule ya sekondari Vikindu(NA SHUSHU JOEL) |
“Walimu wangu nyie tunawategemea sana kutufundishia watoto wetu ili hapo baadae waje kuwa kama tulivyo sie leo hivyo tuwasisitize watoto wetu wawe waangalifu na mali hizi za serikali”Alisema Sanga
Mkuu wa wilaya Mkuranga Filberto Sanga akikagua majengo ya shule. |
Aliongeza
kuwa Serikali imekuwa ikitumia pesa nyingi ili kuhakikisha miundombinu ya
upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi inakuwa ni rafiki hivyo kila mmoja anatakiwa
kutunza thamani za shule kama wao wanavyothaminiwa na serikali.
Kwa upande wake walimu wa majengo wa shule hiyo Bw, Athumani Ally amemwakikishia mkuu huyo wa wilaya kuwa kipindi hiki hakuna mchezo utakaofanyika na hasa juu ya upotevu au kuvunjika kwa thamani za shule na kama mwanafunzi atakayebainika kufanya hivyo basi hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa juu yake.
Aidha
Mwalimu huyo amempongeza mkuu wa wilaya kwa jinsi amekuwa msaada mkubwa kwa
sekta ya elimu kwenye wilaya hiyo kwani amekuwa akitembelea mara kwa mara
mashuleni na hivyo amekuwa akitupatia moyo wa dhati walimu.
Naye Mmoja
wa wazazi waliokuwa wamejitokeza shuleni hapo kuangali watoto wao wamemsifu
mkuu huyo wa wilaya kwa jinsi anavyopambania kukua kwa elimu kwenye wilaya ya
Mkuranga.
MWISHO
0 Comments