DIWANI AWAONGOZA WANANCHI KUTATUA CHANGAMOTO YA BARABARA

 Na Ahmad Nandonde

Kutokana na changamoto kubwa ya ubovu wa miundombinu ya barabara yaliyoharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mengi hapa nchini wakazi wa mitaa miwili ya Zingiziwa na Ngobedi katika manispaa ya ILALA jijini Dar es salaam wameanza kujitolea nguvukazi na mali zao kwa kuanza kukarabati baadhi ya miundombinu ya barabara ili kuondokana na usumbufu wanaoupata pindi wanapotoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.


Wakizungumza na vyombo vya habari wenyeviti wa mitaa hiyo miwili bw. Mohammed Kirungi kutoka mtaa wa Ngobedi na bw. Ally Mkwanda wa mtaa wa Zingiziwa wamesema ujenzi wa makaravati ikiwemo ukarabati unaofanywa kwa kushirikiana na baadhi ya wadau wa maendeleo akiwemo diwani wao sasa unakwenda kupunguza adha hiyo iliyodumu kwa muda mrefu sasa.


Aidha waliongeza kuwa licha ya jitihada hizo za dhati lakini pia ipo haja ya serikali kuongeza nguvu katika kuhakikisha wanaongeza katika kukarabati miundombinu yote ikiwemo ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwani kufanya hivyo kutasaidia ukuaji wa haraka wa kata hiyo.


Walisema hapo awali wanafunzi,walikua kwenye changamoto ya kutohudhuria masomo yao kwa wakati ikiwemo akina mama wajawazito kuwa katika hatari ya kujifungulia njiani kutokana na kutokana na madaraja mengi kusombwa na maji pindi mvua zinaponyesha.


‘’Kuwepo kwa makaravati haya kwa kweli kutatusaidia sana kwani ilikua ni shida kwetu hususani akina mama na watoto ila kwa moyo alionao huyu mdau DK. Charles pamoja na diwani wetu bw. Maige saa tunakwenda kuiona zingiziwa mpya na yenye’’Waliongeza..

Nae diwani wa kata ya Zingiziwa Maige Maganga akaelezea mikakati yake kama kiongozi wa kata hiyo kuwa ni kuhakikisha anawatumiakia vyema wananchi wake kwenye kila hatua kwani dhamira yake ya kuomba uongozi haikua kujinufaisha yeye na tumbo lake bali ni kuhakikisha anawasaidia na kuwainua wananchi ake.

Diwani Mige alienda mbali zaidi na kusema hivi sasa malengo aliyonayo atahakikisha anakwenda mtaa hadi mtaa nyumba hadi nyumba ili kusikiliza kero za wanachi na anachoshukuru miongoni mwa mambo anayoanza nayo ni suala la mawasiliano akimaanisha barabara na vivuko vyake kwa lugha nyepesesi madaraja.

Alisema licha ya kufurahishwa na mwamko mkubwa na mashikamano wa wananchi wake katika kusaidia maendeleo ya kata sasa atahakikisha anaondoka na kero za wananchi ikiwemo barabara mpaka kwenye vikao vya baraza la madiwani ili kuangalia namna ya kupata msaada zaidi.


‘’Kiu yangu kubwa ni kuhakikisha wakazi wa kata ya Zingiziwa wananufaika na uwepo wa serikali ya awamu ya tano iliyochini ya jemedari Dk. John Pombe Magufuli ambayo inaendelea kujipambanua kwa kuwapatia watanzania maendeleo ambayo yatawafanya wajisikie amani ndani ya nchi yao hivi ni wazi kuwa iko radhi kupamnbana usiku na mchana ili kuleta maendeleo ya kweli na vinginevyo’’ Alimalizia Maige….


Mwishoo….

Post a Comment

0 Comments