MWENYEKI UWT ATOA NENO ZITO KWA WANAWAKE.

Na Shushu Joel,  

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) Mkoa wa Pwani Bi,Farida Mgomi amewataka viongozi wote wanaotokana na jumuiya hiyo kuwa nguzo kubwa kwa wanawake nchini ili waweze kuwa kimbilio la wanawake kwa kuwaonyesha fursa mbalimbali.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Farida Mgomi akifafanua jambo kwa wajumbe(NA SHUSHU JOEL)

Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na viongozi wote waliotokana na jumuiya hiyo kuanzia ngazi ya Udiwani Mpaka Ubunge kwa kusudi la kuiweka jumuiya hiyo kuwa na nguvu na kuongeza uthamani.


Aliongeza kuwa kukosekana kwa fursa kwa wanawake kumechangia kutokukua kiuchumi kwa baadhi ya wanawake hapa nchini.


Aidha Bi, Mgomi alisema kuwa anatamani kuona viongozi wa jumuiya hiyo kwa kipindi hiki cha 2020-2025 wanakuwa viongozi wa kuigwa na jamii kwa kuwa mstali wa mbele kwenye kutatua changamoto za wanawake ikiwemo upatikanaji wa mikopo kupitia halmashauri na kuwapatia masoko wajasliamali wadogoqadogo kwa yule mwenye uhitaji.


Pia amewataka wanawake kuonyesha malezi bora kwa watoto wetu ili waweze kutumia nafasi zao vyema na baadae kuja kuwa viongozi kwenye Taifa hili.



Kwa upande wake Mjumbe wa baraza kuu Taifa kupitia Mkoa wa Pwani Bi,Nancy Mutalemwa amewataka madiwani wanawake wakafanya kazi na wanawake mbao ni jeshi kubwa hapa nchini.

Aidha amewasisitiza viongozi kushuka chini kwa chini ili kusaidia jamii za chini.


Naye Mgeni rasmi kwenye mkutano huo ambaye ni katibu wa ccm wilaya ya Mkuranga Ndg Said Kineng'ena amesifu jinsi jumuiya hiyo ilivyojipanga katika kuwasaidia wanawake ili waweze kukuza uchumi wao na kuimarisha Jumuiya kupitia mafunzo yaliyotolewa.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments