VIFO VYA MAMA NA MTOTO KUBAKI HISTORIA MAGU

Na Shushu Joel,Magu.

KUTOKANA na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli tangu iingie madarakani kumekuwa na mabadiliko makubwa katika sekta ya Afya.

Viongozi wa wilaya ya Magu Mkoani Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja kushoto ni Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dr.Maduhu Nindwa na Mwenye suti ya Bluu ni Mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo Ndg George Lutengano(NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii Mganga Mkuu wa wilaya ya Magu Mkoani Mwanza Bw, Maduhu Nindwa alisema kuwa wilaya yetu ilikuwa na changamoto nyingi zilizokuwa zikiwakabili Mama mjamzito na watoto lakini kwa sasa changamoto hizo zimemalizwa na hivyo imebaki historia tu.

Dr Nindwa aliongoza kuwa nguvu kubwa iliyowekezwa na serikali ya Rais Magufuli imekuwa msaada mkubwa kwa wilaya yetu ya Magu kwani kujengwa kwa zahanati kila kijiji na vituo vya Afya kwenye kata kumepelekea  kutokomeza vifo vya mama mjamzito kwa kuwasogezea huduma za Afya karibu na mazingira ya makazi ya wananchi. 

Moja ya majengo ya kituo cha Afya yaliyojengwa na serikali ya awamu ya tano wilayani humo.

Aidha Mganga huyo wa wilaya hiyo ya Magu(DMO) aliwataka wananchi kuendelea kwenda kupata huduma kwenye vituo vya Afya na si kujitibu kienyeji kwani serikali imejithatiri kutoa huduma bora kwa jamii.


Hivyo amewataka wahudumu wa Afya wilayani humo kuendelea kufanya kazi zao za kuwahudumia wagonjwa kwa weledi pindi wanapokwenda kutibiwa waweze kufurahia huduma hizo kwa kuwapa maneno matamu yenye faraja.


Kwa upande wake Ngw'ashi Malimi ni mkazi wa kata ya kahangala kijiji cha Busulwa amempongeza Mganga Mkuu Dr Nindwa kwa jinsi anavyojitolea kwenye kuboresha huduma za Afya katika wilaya yetu ya Magu.


" Kutokana na maboresho hayo ya Afya kina mama tumekuwa na mwamko mkubwa wa kwenda kujifungulia kwenye vituo vya Afya kutokana na upatikanaji wa huduma bora" Alisema

Moja ya Jengo la kituo cha Afya wilayani humo.

Aidha amewataka wananchi wenzake kuendelea kufuata maagizo ya serikali juu ya kulinda miundombinu ya vituo vyetu vya Afya ili vidumu miaka mingi.


Naye Masanja Juma amesifu serikali ya awamu ya Tano kwa jinsi inavyojitahidi kufanya kazi za kuwahudumia wananchi na hasa wanyonge.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments