Na Shushu Joel
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani Mhe Ridhiwani Kikwete ameteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya kudumu ya Kanuni za Bunge na kwenye kamati ya sheria ndogo ndogo.
Kwa uteuzi huo, Mbunge Kikwete atakuwa na majukumu yakusimamia Kanuni, kurekebisha na kufafanua kanuni na sheria zilizogatuliwa kisheria.
Wabunge wapo Dodoma kwa ajili ya vikao vya Kamati vinavyotarajiwa kuanza leo ambapo watapewa mafunzo kabla ya kuanza utekelezaji wa majukumu yao katika Mkutano wa pili wa Bunge la kumi na mbili lilipangwa kuanza 02,February 2021.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Chalinze
0 Comments