WAKAZI WA KIBAMBA WATAKIWA KUCHANGIA SH 3000. UKUSANYAJI TAKA KATIKA MAENEO YAO.

Na. Harold Shemsanga. Kibaha

Wananchi wa eneo la kibamba wilaya ya kisarawe wametakiwa kuchangia Ada ya ukusanyaji wa takataka zinazokusanywa na Mkandarasi kiasi Cha sh 3000 kwa mwezi Ili kuondoa takataka zinazo zagaa katika maeneo mbalimbali ya kibamba.

Baadhi ya takataka zikiwa zimetupwa ovyo mtaani.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kibamba Sembuli Mgendi ameyasema hayo katika mkutano Mkuu wa Mtaa wa Kibamba uliofanyika mjini humo.


 Amesema amepokea malalamiko kutoka kwa Mkandarasi anae kusanya taka hizo kushindwa kukusanya fedha hizo kutokana na baadhi ya wakazi kukataa kuchangia kiasi hicho Cha 3000.


"Ndugu wananchi kiasi kilicho pitishwa na manispaa ya sh 3000 ni gharama ambazo kila mkazi atazimudu na mkumbuke  kukaa na takataka kunaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu, nashauri kila mtu atoe hela ili Mkandarasi aendelee na kazi" alisema mwenyekiti wa serikali ya Mtaa kibamba


Hata hivyo wananchi hao wamemlalalmikia Mkandarasi kushindwa kukusanya taka kwa wakati kwani kwa mujibu wa mkataba anatakiwa apite mara nane lakini hupita Mara nne kwa mwezi hivyo kuwa sababu takataka kukaa  majumbani kwa muda mrefu.


Mmoja ya wakazi hao ni Ibarahim Mwakimomo amesema hawakatai kutoa Ada ya ukusanyaji uchafu bali ni kutokana na Changamoto alizo nazo Mkandarasi ambae amekuwa hatimizi wajibu wake wa kuchukua taka ambazo zinabaki kuwa kero kwao.


Kwa upande wake Mkandarasi Mshana amesema yeye anatupiwa lawama bila kujua shida ni nini lakini amekuwa akijitahidi kuhakikisha anazoa taka katika eneo Hilo kwa wakati lakini wananchi hawatoi hela huku yeye akiwa na watumishi ambao wanapaswa kupata posho ya kazi hiyo lakini imekuwa tofauti.


"Mimi nimekuwa nikijitahidi kukusanya taka lakini wananchi nao wamekuwa wagumu kuchangia lakini bado sijaacha kukusanya taka katika maeneo yao"


Mwisho

Post a Comment

0 Comments