Na Shushu Joel,Mkuranga
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Waitara amewataka wananchi kujiridhisha na maeneo wanayotaka kununua kwa ajili ya makazi ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza.
Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira) Mwita Waitara mbele akiangalia moja ya kiwanda kilicho karibu na makazi ya wananchi.
Waitara
ametoa kauli hiyo alipotembelea kiwanda kinachotengeneza nondo cha Fujian
Hexingwa Co. Limited kilichopo Kisemvule Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.
Alisema
kuwa kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa baadhi ya wananchi wakilalamikia
uchafuzi wa mazingira hususani moshi unaotoka katika baadhi ya viwanda
vinavyozunguka makazi ya watu ikiwemo kiwanda cha Fujian.
“Maeneo
yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda yawe ya viwanda sasa wananchi wakivamia
maeneo haya inakuwa kichaka cha malalamiko na kutaka kulipwa fidia, Idara za
Mipango Miji zielimishe wananchi kuhusu maeneo hayo yametengwa kwa shughuli
gani badala ya kuwaacha wajenge halafu waje kulalamika”.
“Kama
ikitokea mtu ameingilia kiwanda akilalamika hatutamsikiliza, mtu lazima
ajiridhishe je ni kihalali? Kitu gani kimepangwa kujengwa katika eneo hilo,”
alisisitiza Waitara.
Aidha Naibu Waziri huyo aliwataka wamiliki wa viwanda kuajiri wataalam wa mazingira ili waweze kushauri wenye viwanda kuzingatia taratibu kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004.
Katika
hatua nyingine, aliagiza Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filberto Sanga
asimamie wananchi waliojenga kando ya kiwanda hicho watakapolipwa fidia ifikapo
Machi 30 mwaka huu, wawe wameondoka katika eneo hilo ili waondokane na kelele
zitokanazo na shughuli zinazofanyika kiwandani hapo.
Vile
vile, Naibu Waziri huyo aliwaagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira (NEMC) wafanye ukaguzi wa mara kwa mara katika kiwanda hicho ili
kuhakikisha kuwa kinazingatia Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 ili kupunguza
uchafuzi wa mazingira utakao weza kujitokeza.
Kwa
upande wake Mkuu huyo wa Wilaya hiyo alisema kuwa malalamiko ya wananchi
yanatokana na baadhi ya wananchi kununua viwanja kiholela ambavyo havijapimwa
na Halmashauri ya Wilaya na viko karibu na maeneo ya viwanda.
Pia alitumia nafasi hiyo kuwaelekeza wataalamu wa ardhi na mipango miji kutoka wilaya hiyo kuanza kutenga na kupima maeneo yatakayotumika kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda wilayani humo
Sanga
alimshukuru Naibu Waziri Waitara kwa kufanya ziara ya kutembelea wilaya hiyo
hususan katika kiwanda hicho ili kujionea changamoto za kimazingira kwa
wananchi wanazonguka kiwanda hicho.
Kiwanda
cha Fujian Hexingwa Co. Limited kinalalamikiwa na baadhi ya wananchi kuwa
kinatoa moshi mzito pamoja kelele hali inayoathiri mazingira na afya za wakazi
waishio karibu na kiwanda hicho.
MWISHO
0 Comments