Mkuu wa mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko ametoa wito kwa wananchi wote ndani ya Mkoa wa Katavi kujitokeza kwa wingi katika ziara ya Waziri Mkuu Dr.Mwigulu Nchemba inayotarajiwa kuanza hivi karibuni Mkoani humo
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake leo March 11,2026,RC Mrindoko ameeleza kuwa Waziri Mkuu Dr.Mwigulu Nchemba atawasili kesho March 12,2026 Mkoani Katavi na kuanza ziara March 13,2026 hadi March 16 katika Wilaya zote tano za Mkoa wa Katavi.
Aidha,amesema kuwa katika ziara hiyo,Waziri Mkuu Dr.Mwigulu Nchemba atatembelea,kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayoendelea kutekelezwa ndani ya Wilaya hizo pamoja na kufanya mikutano ya hadhara kusikiliza kero za wananchi.
Katika hatua nyingine,RC Mrindoko amewataka wananchi kuendelea kuilinda amani na utulivu ndani ya Mkoa wa Katavi pamoja na kushiriki maeneo yote ya miradi na mikutano ya hadhara atakayoifanya Waziri Mkuu Dr.Mwigulu Nchemba.
Nao wakazi wa Manispaa ya Mpanda akiwepo Hamida Salum amesema yupo tayari kumpokea Waziri Mkuu Dr.Mwigulu Nchemba kwani anafurahishwa na utendaji wake wa kazi kote alikopita na namna anavyosikiliza kero za wananchi.
MWISHO .
0 Comments