DC RUFIJI AWAONYA WAZAZI WANAOWAACHISHA WATOTO SHULE

Na Shushu Joel

 Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele ameagiza kukamatwa kwa Vijana na Wazazi wote wenye watoto ambao wana umri wa kwenda shuleni Watakaonekana wanafanya biashara maeneo ya stendi na maeneo mengine muda wa masomo .

Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele akisisitiza jambo katika mkutano wa wadau wa elimu(NA SHUSHU JOEL)

Ameyasema hayo katika kikao Cha Wadau wa Elimu kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri Wilayani Rufiji.


Sanjari na hilo, amewaonya Wazazi wanaomaliza kesi za mimba kwa Watoto wa shule bila kwenda mahakamani na kuwageuza mabinti hao sehemu ya kujipoatia kipato.


Pia ameitaka Jamii kukemea swala la Wazazi kuwaacha Watoto wanaosoma kulea familia Jambo linalozorotesha maendeleo yao kielimu.


Gowele ameendelea kuhamasisha Jamii na Wadau mbalimbali wa Elimu kuendelea kuunga Mkono  juhudi za Serikali ya awamu ya sita  katika uboreshaji wa miundombinu ya Elimu kwa Shule za  Msingi na Sekondari  huku akishukuru Bank ya NMB , CAMFED  pamoja na Mdau kutoka Korea kwa misaada wanayotoa katika kuboresha Elimu Wilayani humo.


 Sambamba na hayo, amemshukuru  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake kubwa anazozifanya kwa kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya ya Rufiji

MWISHO

Post a Comment

0 Comments