Na Shushu Joel Bagamoyo.
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amezidi kusononeshwa na wananchi wa Mkoa huo kuendelea kuwa masikini huku Mkoa wa Pwani ukiwa na kila Raslimali ya kuwafanya wakazi wa Mkoa huo kuweza kuwa matajiri.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akisisitiza jambo kwa wananchi wa wilaya ya Bagamoyo(NA SHUSHU JOEL)
Akizungumza
na wananchi wa wilaya ya Bagamoyo Kunenge alisema kuwa Mkoa wa Pwani umejaaliwa kuwa na kila kitu ambacho
kitamfanya mkazi wa eneo fulani kuwa ni mtu mwenye kipato cha kutosha kwa
kupitia raslmali zinzomzunguka mkazi huyo.
"Pwani
kuna kokoto bora za kutengeneza mabarabara, vituo vya utalii,Ardhi yenye
rutuba, viwanda, Bwawa la Mwalimu Nyerere
na vingine vingi vipo kwenye Mkoa wetu kwanini tunakuwa masikini
"Alisema Kunenge.
Hivyo Mkuu
huyo wa Mkoa amewataka wananchi wote wa Mkoa huo kuhakikisha wanachangamkia
fursa zilizopo ndani ya Mkoa kwa kujiongezea kipato zaidi.
Aidha
aliongeza Mkoa huu una vitu ambavyo uwezi kuvipata sehemu yeyote ile kwa mfano
Makumbusho ya Bagamoyo,Bahari ya blue huko Mafia hivi vyote ni fedha sema ni
ubunifu tu wa jinsi gani unaweza kuivuna pesa hizo.
Kwa upande
wake Haji Juma mkazi wa kata ya Nia Njema amempongeza mkuu wa mkoa kwa ziara
yake ya kata kwa kata katika wilaya ya Bagamoyo huku akisisitiza ni kweli
wananchi wa mkoa huu kuwa masikini ni kujitakia tu.
Aidha
aliongeza kuwa ni halali Mkuu wa Mkoa wetu Kunenge asononeshe na umasikini wetu
huku Mkoa wetu ukiwa na Raslimali nyingi na za kutosha za kumfanya mwananchi
kuweza kuwa na uwezo mkubwa wa kipato.
“Elimu ya Mkuu
wa Mkoa ni funzo kwetu hivyo wananchi wenzangu tujifunze kupitia maneno ya Mkuu
wetu wa Mkoa kwani ni siku chache tu tangu kuwa kiongozi lakini kaona jinsi
gani wana Pwani tunavyoshindwa kutumia fursa”Alisema Haji.
Naye
Mwanaisha Mwalami amemsifu Mkuu wa Mkoa kwa kuwavuta masikio na kusema kuwa
kweli Kunenge ni kiongozi wa maono ya mbali sana.
Pia
amewataka wanawake wote Mkoa huo kuyadadafua au kuyatafakali maneno hayo mazito
ya Mkuu wa Mkoa juu ya uwepo wa wingi wa raslimali kwenye Mkoa wetu cha ajabu
wananchi wake ni masikini kweli inauma.
MWISHO
0 Comments