Na Shushu Joel
WANANCHI wa wilaya za Mkoa wa Pwani wamempongeza Mkuu wa Mkoa huo Abubakar Kunenge kwa juhudi zake kubwa anazozifanya kwa wakazi wa maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akisisitiza jambo kwa wananchi(NA SHUSHU JOEL) |
Kunenge amekuwa akijitoa kwa uwezo wa akili zake zote ili kjhakikisha Mkoa wa Pwani unakuwa na maendeleo makubwa na ya kuigwa nchini na nje ya nchi.
Wakizungumza kwa wakati tofauti tofauti na Mwandishi wa habari wa online TV na Blog ya HABARI MPYA wananchi hao walisema kuwa Mkuu wetu wa Mkoa amekuwa akijitoa katika masuala mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha maendeleo katika Mkoa wa Pwani yanakuwa kwa upesi ili kila mkazi wa Mkoa huu anakuwa tajiri.
Kheri Majaliwa ni mkazi wa wilaya ya Mkuranga alisema kuwa Mkuu wa Mkoa amekuwa akiwahamasisha wananchi kujikita katika uzalishaji wa miradi ya maendeleo huku serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ikichanja Mbuga.
Aidha aliongeza kuwa tangu Mkuu wa Mkoa Kunenge kuja Pwani wilaya ya Mkuranga imekuwa na hamasa kubwa ya uibuaji wa miradi ya maendeleo na hasa katika nyanja za elimu,afya na ongezeko la viwanda .
Naye Khadija Ibrahim mkazi wa Bagamoyo alisema kuwa Mkuu wa Mkoa Kunenge amekuwa msaada mkubwa kwa jamii kwani mbali na nafasi yake ya uongozi amezidi kuwa Baba wa Mkoa wa Pwani kutokana na uongozi wake uliotukuka kwa wananchi.
Aidha aliongeza kuwa ni kipindi kifupi tu cha muda aliongoza Mkoa wetu lakini Pwani imekuwa na mabadiliko makubwa si tu kwa serikali bali hata wananchi tumeanza kuona neema ya maendeleo kwani mengi yalikuwa hayawezekana lakini uwepo wa Kunenge umekuwa nu suluhisho kubwa kwetu.
"Kweli wananchi wa Mkoa wa Pwani chini ya Mkuu wetu wa Mkoa Abubakar Kunenge mabadiliko makubwa yanaonekana ndani ya Mkoa wetu kweli mfupa uliomshinda fisi umeanza kupolomoka"Alisema Bi'Khadija.
Aliongeza kuwa ni vyema kila .wananchi akamuunga mkono mkuu wetu wa Mkoa kwa yale tuliyokuwa tukiyahitaji yafanyike hapa Pwani yanafanyika.
Shabani Manda ni Diwani wa kata ya Tengelea iliyoko wilaya ya Mkuranga amemsifu Mkuu wa Mkoa Abubakar Kunenge kwa utendaji kazi wake kwani Mkoa wa Pwani ulikuwa nyuma sana lakini kwa sasa hatua kali za maendeleo zinaonekana ndani ya uongozi wake chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya sita Samia Suluhu Hassan.
"Yanayofanyika yanaonekana na yale ambayo yalishindwa kufanikiwa kufanyika yanafanyika "Alisema Manda
MWISHO
0 Comments