Na Shushu Joel, Kibaha.
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amewataka wakuu wa wilaya zote za Mkoa huo kuhakikisha wanatumia nafasj ya kuzitangaza wilaya zao kwa fursa za utalii zilizomo ndani ya wilaya zao.
![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya zote za Mkoa wa Pwani(NA SHUSHU JOEL) |
Rai hiyo ameitoa alipokuwa katika hifadhi ya Saadan iliyopo wilaya ya Bagamoyo Mkoa humo kwa kusema kuwa kumekuwa na changamoto ya viongozi wa serikali kutozitangaza fursa za kitalii zilizopo ndani ya wilaya na hivyo kupelekea kwa baadhi ya watanzania kutokujua vitu hivyo sehemu gani.
Aliongeza kuwa Pwani ni Mkoa uliobalikiwa kwa kila kitu hivyo ni lazima vitu hivyo tuviseme kwa jamii ili Taifa lijue ili watu kutoka sehemu mbalimbali za ndani ya nchi na nje waje kujionea na kujifunza pia.
"Kwa mfano wilaya kama Bagamoyo hakuna isipofahamika duniani lakini je inafahamikaje kwa makaratasi tu na si watu kuja kujionea kile kilichopo kwenye hayo makaratasi sasa Mkuu wa wilaya hiyo hakikisha unahamasisha watu wafike Bagamoyo ili wafike na kujifunza mambo ya kale yalivyokuwa"Alisema Kunenge
Aidha wilaya nyingine ni Mafia huku kuna bahari yenye maji ya Bluu kitu ambacho duniani kipo huko tu hivyo ni fursa ya kipee kabisa,pia wilaya Rufiji napo kuna utalii wa kutosha kwani kuna hifadhi ya Mwalimu Nyerere pia kuna Bwawa kubwa na lenye uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme.
Hivyo niwaombe wakuu wa wilaya zote katika Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanachangamkia fursa za uwepo wa utalii huo kwenye hayo maeneo pia itatuingizia fedha za kutosha na hivyo itapelekea kuwepo kwa maendeleo ya kutosha kwa wananchi.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zaynabu Issa amempongeza mkuu wa Mkoa kwa kuwafungua macho viongozi wenzake kwa kuwaonyesha namna gani wilaya zinavyoweza kujiongezea kupata kipato kupitia fursa za ndani.
Hivyo niwatake wananchi wa wilaya yangu kutembelea kwenye hifadhi ya Saadan kwa lengo la kujionea wanyama mbalimbali waliopo Kwenye hifadhi hiyo, Pia niwakumbushe kutembelea kwenye makumbusho ya mahali ambapo watumwa walifikishwa kabla ya kusafirisbwa.
Naye Ramadhani Juma ambaye ni mmoja wa wafanya kazi katika hifadhi hiyo alisema kuwa ni kweli idadi ya watalii wa ndani ni ndogo kuliko wa nje na hii ni kutokana na watanzania wengi hatuna utaratibu wa kutembea hifadhi zetu.
"Kutokana na jambo hili sasa kupewa kipahmbele na Mkuu wa Mkoa naamini idadi kubwa ya watalii itaongezeka maana kuna mafunzo ya kila aina"Alisema Jumaa
MWISHO

0 Comments