Na Shgushu Joel,Pwani
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesisitiza mabaraza ya ardhi kusimamia sheria, kutenda haki, kusikiliza Pande zote na kuepuka mgongano wa maslahi katika kushughulikia migogoro ya ardhi.
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akisisitiza jambo kwa viongozi wa mabaraza ya Ardhi mara baada ya kura kiapo(NA SHUSHU JOEL) |
Msisitizo huo ameutoa alipokuwa akiwaapisha wajumbe wanna wa Baraza la ardhi la Wilaya ya Kisarawekwenye ukumbi wa Mkuu wa Wilaya hiyo.
Akiwaapisha wajumbe hao Kunenge alisema kuwa lengo la Serikali ni kusogeza huduma karibu na Wananchi hivyo baraza la hilo la kisarawe limeundwa ili kutimiza azma hiyo.
"Wilaya ya Kisarawe hapo awali haikuwa na Baraza la Ardhi, Wananchi walilazimika kwenda Wilaya ya Kibaha pindi wanapopata Migogoro ya Ardhi, sasa wasaidieni.” Alisema Kunenge.
Mkuu huyo wa mkoa pia aliwafunda wajumbe hao kutotekeleza majukumu yao kwa kudai rushwa akisema “hawa wananchi ambao wanakuja kwenye Baraza la Ardhi hawana fedha, wengine wamevamiwa ardhi yao na watu wenye uwezo wa kifedha, tuwasaidie Wananchi wetu kupata haki yao”.
Kunenge amewaeleza wajumbe hao kuwa kitendo cha kuwaapisha maana yake pia ni kuwa atawafuatilia utendaji kazi wao na akawahimiza Viongozi na Watendaji wa Serikali kuhakikisha kuwa kesi zinapungua na zikifika kwenye Mabaraza kesi hizo ziishe mapema kwasababu ya ushahidi mzuri kutoka kwa Watendaji na Viongozi wa Serikali.
Kuhusu Mabaraza ambayo hayafanyi kazi, Mkuu huyo wa Mkoa amemuagiza Katibu Tawala Mkoa kufuatilia na kuhakikisha kuwa Mabaraza ya Ardhi ya kata ambayo hayafanyi kazi yanafanyiwa utaratibu wa kisheria ili yafanye kazi.
"Mkoa wa Pwani una Changamoto kubwa ya Migogoro ya Ardhi, Mabaraza ya Ardhi ya Nyumba za Wilaya na Kata zinatakiwa kuwa jibu" amewaeleza Kunenge.
MWISHO
0 Comments