Na Shushu Joel, Chalinze.
SERIKALI ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeshusha neema kubwa kwa wananchi wa Jimbo la Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya maendeleo .
![]() |
Waziri wa TAMISEM katikati Ummy Mwalimu akizungumza mbele ya wananchi wa jimbo la Chalinze mara baada ya kuahidi pesa zaidi ya Bilion 4 za miradi ya maendeleo. |
Akizungumza katika ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo Waziri wa Tawala za Mikoa na Seriali za Mitaa(TAMISEMI) Ummy Mwalimu alisema kuwa Serikali ya awamu ya sita itatoa fedha zaidi ya Bilion 4 kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Jimbo la chalinze.
"Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi chalinze,Miluon 40 kwa ajili ya madarasa mawili,Milion 600 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari,million 370 kwa ajili ya vifaa Tiba,Bilion 2 kwa ajili ya Barabara za Tarura na million 400 kqa ajili ya vifaa Tiba vya zahanati" Alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy alisema kuwa halmashauri ya Chalinze imekuwa ni miongoni mwa halmashauri zinazofanya vizuri katika mapato ya ndani na ndio maana imekuwa ikipjga hatua kubwa katika maendeleo.
Mbali na utoaji wa pesa hizo Waziri Ummy amewakumbusha watendaji wote wa serikali kuhakikisha wanakuwa wabunifu wa vyanzo vya mapato kama ilivyofanikiwa halmashauri ya Chalinze.
Aidha aliongeza kuwa ni vyema sasa wakurugenzi wakaja kujifunza chalinze kwani serikali ilitoa Bilion 1 kwa ajili ya majengo 3 lakini wamejenga 5 hii no hatua nzuri na yenye kuleta tija kwa maendeleo ha Taifa letu.
"Wananchi niwatahadhalishe na uongo unaendelea eti Rais Samia Suluhu Hassan hanamponho wa kuondoa elimu bure hao watu wapuuzwe kwani mpaka sasa serikali tumetoa pesa za kutosba kwa halmashauri zetu kwa ajili ya elimu bure"Alisema Waziri Ummy
Kwa upande Mbunge wa Jimbo hilo Ridhiwani Kikwete amempkngeza Waziri Ummy kwa jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa kwa maendeleo ya Taifa hili na hasa kwenye sekta ya Afya,Elimu na Miundombinu na hii inaonyesha Rais Samia Suluhu Hassan hakukosea kuweka katika nafasi hiyo.
Aidha Kikwete aliongeza kuwa fedha hizo ziliyolewa na serikali ni ishara tosha kabisa kuwa Mama Samia Suluhu Hassan hataki mchezo katika maendeleo ya wananchi wa Tanzania.
Aidha amewataka wananchi wa Jimbo lake kuendelea kumuombea Dua Rais Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuwa na Afya nzuri kwani tangu achukue kijiti amekuwa akiongozi vyema Taifa hili.
"Wengi tumemshuhudia Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa 76 wa UN alivyotuwakilisha vyema kwenye mkutano huo na hasa alivyosisitiza suala la usawa na mahusiano mazuri" Alisema Kikwete
Salma Juma Mkazi wa Chalinze ameipongeza serikali ga awamu ya sita kwa jinsi ambavyo imekuwa karibu na wananchi na kubwa ni katika ufanikishaji wa miradi mikubwa na midogo.
Hivyo hii ni kweli kabisa mwananmke anaweza kuwa msaada mkubwa katika jamii kama inayoonyeshwa na Rais weth Samia Suluhu Hassan katika uchapakazi wake ,Mama endelea Sisi wanawake wenzio tuko nyuma yako.
MWISHO
0 Comments