Na Shushu Joel,Busega
MBUNGE wa jimbo la Busega Mkoani Simiyu Simon Songe amewataka wananchi wa jimbo hilo kila mmoja kwa wakati wake kuhakikisha anakwenda kupata chanjo ya covid 19.
![]() |
Mbunge wa Jimbo la Busega Mhe:Simon Songe akiwashuudia vijana wakipata chanjo siku ya fainali ya SONGE CUP(NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza
na wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye fainali ya mashindano ya SONGE CUP
yaliyozikutanisha timu za kata ya Kiloleli na Shigala Mbunge huyo alisema kuwa
unapopata chanjo ya Corona unaepukana na mambo mengi hivyo ni jukumu la kila
mmoja wetu kuchangamkia fursa hiyo ya chanjo inayotolewa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan bila malipo.
Aidha alisema kuwa kuna watu wamekuwa wakipotosha juu ya chanjo hii ya Covid 19 nawaombeni wananchi wenzangu watu wa namna hiyo ni bora mkawapuuza kabisa kwani chanjoi hizo hazina madhara ya aina yeyote ile katika mwili wa binadamu kwani ni salama kwa Afya zetu.
“kila mmoja
wetu amemuona kiongozi wetu,Mama yetu Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassan amekuwa wa mfano kwa kupata chanjo na pia
ametuhakikishia chanjo hizo ni salama salimini hivyo niwaombe twende
tukachanje”Alisema Songe
Aidha Mbunge
huyo aliwashauri wataalamu wa Afya kuendelea kutoa elimu kwa jamii kwani
wananchi wako tayari kupata chanjo lakini tatizo limekuwa ni kufikiwa kwao
hivyo ni vyema tukatengeneza utaratibu wa kutoa elimu kila panapokucha iwe
nyumba kwa nyumba au namna nyingine yeyote ile itakavyokuwa.
Kwa upande
wake kiongozi wa timu ya Kiloleli FC Christopher Vincent amempongeza mbunge
huyo kwa namna jinsi alivyojipanga katika mashindano hayo kwani yamekuwa ni ya
pekee kutoknana jinsi yalivyoandaliwa kuanzia huduma ya utoaji wa elimu ya
Covid 19 na mambo mengi mengi.
Aliongeza
kuwa kutokana na elimu tuliyoipata
kutoka kwa wataalamu wa Afya imetujengea uwezo mkubwa na uelewa wa hali
ya juu kuhusu umuhimu wa chanjo ya Covid 19.
“Tumekuwa
washindi wa SONGE CUP leo katika Nyanja mbili ambazo ni kombe pamoja na elimu yay a chanjo ya corona kweli Mbunge
wetu anastahili pongezi sana”Alisema Vincent.
Kwa upande
wake Mganga Mkuu wa wilaya ya Busega Godfrey Mbagali amempongeza Mbunge kwa
jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa katika sekta ya Afya kwani kila anapokwenda
ajenda yake amekuwa akiwataka wananchi wenye nafasi ni bora wakapata chanjo ya
Covid 19 ni salama na ndio maana hata Rais wetu amekuwa wa kwanza kupata kinga
ya ungonjwa huo.
Aidha
Mbagali amewatoa hofu wananchi kuwa hakuna tatizo lolote lile kuhusu chanjo
kwani iko vizuri na hakuna madhara yeyote yale yatokanayo na chanjo hiyo.
MWISHO
0 Comments