MGALU AWATAKA WANAWAKE KUMSEMEA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN.

Na Shushu Joel, Kibiti.

MBUNGE wa  Viti maalum kwa tiketi ha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokea Mkoa wa Pwani Subra Mgalu amewagaka wanawake kote nchini kujitokeza na kumsemea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa yale anayowafanayia watanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani Mhe.Subra Mgalu akisisitiza jambo (NA SHUSHU JOEL)

Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na umati wa wanawake wa wilaya ya Kibiti katika moja ya mikutano iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Twaha Mpembenwa.

Mgalu alisema kuwa ni vyema kila Mwananmke akajitokeza kumsemea Rais wetu ambaye ameonyesha nia njema na ya dhati katika ufanikishaji wavmaendeleo makubwa na yenye tija katika Taifa letu.

"Kumbukeni wanawake tuko wengi hivyo kama tukimsemea mazuri Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kila tunapokuwa itasaidia sana katika jamii kuondoa dhana Mwanamke hawezi kitu ambacho kimepitwa na wakati" Alisema Mgalu 

Aidha Mgalu aliongeza kuwa miongoni mwa sehemu ambazo zinazidi kunufaika na Rais Samia Suluhu Hassan ni pamoja na wilaya ya Kibiti kwani Bwawa la Umeme kubwa katika nchi za Afrika Mashariki lipo Kibiti,Maji ya uhakika yanaletwa Kibiti kutoa Mto Ruvu hospital ya wilaya,vituo vya Afya na zahanati za kutosha zinajengwa hapa kwenda tayari fedha zipo. 

Mhe, Mbunge viti maalum Subra Mgalu kushoto akiteta jambo na katibu Tawala Mkoa huo Mwanasha Tumbo

Kwa upande wake Bi, Aisha Ally(64) MkaI wa Kibiti amempongeza Mgalu kwa juhudi zake za kumsemea Rais Samia Suluhu Hassan kwa yale anayoyafanya Katika nchi yetu.

Aidha amemtaka kuendelea kutoa elimu hiyo kwani tulio wengi tunafikili kazi ya kumsemea Rais ni ya Wabunge tu kumbe hata sie watu wa chini tunapaswa kumsemea Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan. 

Naye Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ya kina mama kupewa elimu ya kuondokana na umasikini iliyoandaliwa na Bank ya NBC ambaye ni katibu tawala wa Mkoa Mwanasha Tumbo amempongeza Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa uchapkazi kazi wakehuku pia akimsifu Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Pwani  kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe, Shbra Mgalu ambaye amezidi upambanaji Kwa wananchi jambo ambalo limekuwa likifanywa na yeye tu na hii yote ni mapenzi ya dhati aliyonayo kwa Rais Mama Sàmia Suluhu 

MWISHO

Post a Comment

0 Comments