Na Shushu Joel,Bagamoyo
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amemtaka mkandarasi anayejenga soko la samaki katika wilaya ya Bagamoyo Mkoani humo kuhakikisha anakamilisha ujenzi huo ndani ya mkataba kama walivyokubaliana.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akisisitiza jambo kwa mshauri wa mradi (NA SHUSHU JOEL)
Akitoa
maagizo hiyo Kunenge alisema ni lazima soko hili likamilike kwa wakati kama
ilivyokuwa imekusudiwa na serikali ili wananchi wa hapa waanze kunufaika na
serikali yao ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
“Naagiza
ujenzi wa hapa uwe usiku na mchana kwani siku zilizobaki ni chache sana na
wananchi wanahitaji waanze kutumia soko hili kwa wakati”Alisema Kunenge.
Aidha
aliongeza kuwa wananchi wa Bagamoyo asilimia kubwa wanategemea bahari kuendesha
shughuli zao za kila siku kwani wengine ni wavuvi na wengine ni wasafirishaji
hivyo nahitaji soko hili likamilike kwa haraka ili wananchi hawa waanze
kujiingizia kipato kutokana na sughuli zao za bahari.
“Soko hili linatakiwa kukabidhiwa mwezi wa kumi kwenye tarehe za mwanzo hivyo na nataka tarehe usika soko hilo liweze kukabidhiwa kama ilivyokubaliana la sivyo nitawashitaki kwa kuchelewesha huduma muhimu ya wananchi wangu”Alisema Kunenge.
Muonekano wa soko la samaki wilayani Bagamoyo ulivyo sasa (NA SHUSHU JOEL)
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa CCM wialaya ya Bagamoyo Sharifu Zahoro amempongeza mkuu huyo
wa Mkoa kwa jinsi alivyotoa maamuzi ya kukamilishwa kwa soko hilo la samaki ili
wananchi wa Bagamoyo waweze kunufaika kwa haraka pia halmashauri kuweza
kujiongezea kipato”Alisema Zahoro
Aidha alisema kuwa wao kama upande wa chama ni furaha kubwa kwao kukamilika kwa miradi kya wananchi kwani pindi wanapoenda kwa wananchi wanakuwa nayo ya kujivunia kama chama.
Naye Ally
Mbarouk mkazi na mvuvi wilaya ya Bagamoyo alisema kuwa wao kama wavuvi
wamefurahi kumuona mkuu wa Mkoa anafika kwenye soko hilo walilolisubilia kwa
kipindi kirefu kwa ajili ya kuhakikisha usalam wa shughuliu zao.
Pia
aliongeza kuwa ujio wa kiongozi huo kutapelekea kukamilika kwa haraka kwa soko
hilo na hivyo shughuli za uvuvi kuendelea kwa kiwango cha hali ya juu.
MWISHO
0 Comments