MGALU AWAMWAGIA SIFA VIJANA WAZALENDO.

Na Shushu Joel, Rufiji.

MBUNGE wa Viti maalum Mkoa wa Pwani Mhe. Subra Mgalu amewapongeza vijana 1700 Wazalendo waliotembea kwa miguu tokea Mkoani Dar es Salaam mpaka  wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani wakiwa na lengo la kuonyesha Uzalendo.

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani Subra Mgalu akiwa wa vijana wa Bega kwa Bega(NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokelewa kwa vijana hao Mhe. Mgalu alisema kuwa vijana hao wameonyesha uzalendo mkubwa kwa nchi yao kwa matembezi hayo ya dhati ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

"Vijana hao Wazalendo wametuheshimisba sana Jumuiya ya Umoja wa wanawake Tanzania kwa kuonyesha Uzalendo wao wa kutembea na kuonyesha kumuenzi aliyekuwa mwasisi wa Jumuiya hiyo  Hayati Bibi Titi Mohamed " Alisema Mgalu.

Kwa kweli sherehe hizi zimefana kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa ngeni rasmi katika maadhimisho hayo yaliyofanyika wilaya Rufiji" Alisema Mgalu 

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wilaya ya Kibitu  Juma Ndaluke ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa matembezi hayo amemshukuru Mhe. Mgalu kwa kuonyesha upendo wake kwetu na hata kufikia hatua ya kuja kushuhudia matembezi yetu.

" Huu ni Uzalendo wa hali ya juu pia amewatia moyo vijana hao hata kuona kuwa na wao wanathaminika kwa viongozi"  Alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha amewataka vijana hao kuendeleza  uzalendo huo kwa Taifa  letu ambalo waasisi wake walituhasa kupenda nchi yetu kwani hatuna nchi nyingine tofauti na Tanzania.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa wanawake Tanzania Taifa Bi,Gaudencia  Kabaka amewasifu wanawake wa Mkoa wa Pwani kwa kuwa na Mwanamke shupavu ambaye aliongoza mapambano ya Mwanamke katika Taifa hili Hayati Bibi Titi Mohamed ambaye makazi yake yalikuwa wilaya ya Rufiji..

Kuanza kwa maadhimisho haya ya kumuenzi Bibi Titi Mohamed kitaifa ni mwanzo wa mwendelezo wa heshima hiyo kwa kiongozi wetu huyo.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema kuwa Hayati Bibi Titi Mohamed alianza lakini Mama Samia Suluhu Hassan anaendeleza gurudumu hilo la kuonyesha kuwa Mwanamke anaweza. 

MWISHO

Post a Comment

0 Comments