“MTUMIENI RC KUNENGE ATAWAVUSHA”MAKAMU WA RAIS DKT MPANGO.

Na Shushu Joel,Kibaha

MLEZI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdor Mpango amewataka viongozi na wananchi wa Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanamtumia ipasavyo Mkuu wa Mkoa huo Mhe:Abubakar Kunenge kwani ni mtu mwenye uchu wa maendeleo.

Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge(NA SHUSHU JOEL)

Rai hiyo ameitoa hivi karibuni  alipokuwa katika moja ya vikao vyake vya kuzungumza na viongozi mbalimbali wa CCM alipokuwa amekwenda kujitambulisha kuwa yeye ndiye mlezi wa Mkoa huo kwa upande wa chama cha mapinduzi(CCM)

Alisema kuwa maneno hayo mbele ya  wana chama wa chama cha mapinduzi (CCM) kupitia viongozi wao kuanzia ngazi ya kata mpaka Mkoa Makamu wa Rais Dkt Mpango alisema kuwa kati ya wakuu wa Mikoa wenye uchu wa kuona wananchi wake wananufaika ni huyu wenu hapa.

Aidha alisema kuwa utendaji wa kazi zake ni za kimakini na zenye uhakika kwa jamii inayomzunguka hivyo niwaombe muwe mnamshirikisha kwa kila jambo hili muweze kufika mbali zaidi ya hapa mlipo.

“Namjua Mkuu wenu wa Mkoa Kunenge ndio maana nawaombeni muwezi kumtumia katika Nyanja mbalimbali za kukuza uchumi wa mkoa wetu kwani ni mtu mwenye maono ya mbali”Alisema Dkt Mpango.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) wilaya ya Bagamoyo Sharifu Zahoro amempongeza mkuu wa Mkoa kwa jinsi ambavyo viongozi wakubwa wan chi yetu wanavyotambua utendaji wake wa kazi katika Mkoa wa Pwani.

Aliongeza kuwa ni jambo la kumpongeza Rais wetu wa Jmhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutusaidia wananchi wa Mkoa wa Pwani kwa kuona jinsi gani tunahitaji Mkuu wa Mkoa mwenye hekima busara na uadilifu mkubwa na ulio tukuka  kwa wananchi wake na hasa wanyonge.

Aidha alisema kuwa wananchi wa Mkoa wa Pwani tuna matumaini makubwa kwa kuona Mkoa wa Pwani unakua kiuchumi,kisayansi na kisiasa kutokana na uwepo wa kiongozi makini mwenye kusikiliza changamoto za wakazi wa Pwani na kisha kuzitatua.

“Kwa sasa Mkuu wetu wa Mkoa Ndugu Kunenge yupo kwenye ziara ya kusikiliza kero za wananchi ambapo anakwenda kata kwa kata jambo ambalo hapao awali halikuwepo lakini sasa wananchi wanapatiwa fursa ya kusema kile kinachowakabili na hata kutoa ushauri jinsi gani Mkoa ufanye ili kukuza uchumi kwa kujenga miundombinu mbalimbali” Alisema Sharifu.

Naye Bi,Mwajuma Ally amesifu juhudi za Mkuu huyo wa Mkoa kwa namna jinsi ambavyo amekuwa akipambana na jinsi gani Mkoa wa Pwani unaweza kupiga hatua kwenye masuala mbalimbali ya kimaendelea .

Hivyo kwa niaba ya wanawake tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumleta Kunenge katika Mkoa wa Pwani kwa kusudi la kukuza maendeleo kwa wananchi wote kwani Mkoa huu una kila sababu ya kuwa juu kimaendeleo kutokana na jiografia ya maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Pwani.

Aidha alisema kuwa tangu uwepo wa Mkuu wa Mkoa Kunenge kuwepo kwenye Mkoa wetu manufaa makubwa yameanza kuonekana kwa watu mmoja mmoja na kuongezeka kwa uwekezaji wa viwanda hizi zote ni juhudi binafsi .

MWISHO

 

 

 

Post a Comment

0 Comments