DIWANI KIMARA AONGOZA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU HOSPITAL YA WILAYA

 Na Shushu Joel, Ubungo.

DIWANi wa kata ya Kimara wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es Salaam Mhe. Ismail Mvungi amewaongoza wananchi wa kata hiyo kwenye zoezi la kujitolea Damu na upandaji wa miti kwenye   Hospital ya wilaya hiyo iliyopo kwenye kata yake.

Diwani wa kata ya Kimara Ismail Mvungi akichangia damu katika hospital ya wilaya ya Ubungo(NA SHUSHU JOEL)

Zoezi hilo limeendana na shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kuhamasisha watu kufanya mazoezi,upandaji wa miti na utoaji wa Damu kama walivyofanikiwa wao na wana vikundi mbalimbali wa Joging na wananchi wengine waliojitokeza kwenye zoezi hilo.

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo Diwani huyo alisema kuwa   hospital hii inakwenda kuwa mkombozi kwa Afya zetu wananchi wa kata ya Kimara na wilaya yetu kwa ujumla kutokana na ukaribu wa huduma kwa wakazi hao.

"Tumeamua kufanya hamasa hii ya kupanda miti,kuchangia damu na ufanyaji wa mazoezi kama kuonyesha jamii kuwa viongozi wao tunafanya kazi za kufanikisha maendeleo huku tukiwa na Afya njema" Alisema Mvungi .

Aidha Duwani huyo amewahakikishia wananchi wa kata yake kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inapambana ili kuwaondolea changamoto wananchi wake kwa kuwapatia huduma wanazozihitaji kama vile Miundombinu,Umeme,Maji na huduma za Afya na ndio maana katuletea chanjo ya COVID 19 bure.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dr Peter  Msanya alisema kuwa zoezi lililofanywa na Diwani wa kimara ni ushaidi mkubwa kuwa yuko pamoja na serikali katika kuhakikisha huduma za wananchi zinakuwa za uhakika kama inavyokusudiwa na serikali yetu.

Hivyo nimpongeze Diwani kwa kuhamasisha wananchi waweze kujitokeza kuchangia Damu na kupanda miti katika eneo hilo la hospital ya wilaya.

Aliongeza kuwa Afya ni jambo la muhimu sana na ndio maana tunawataka wananchi kufanya mazoezi kwa lengo kuepukana na magonjwa nyemelezi yanayotokana na kutokufanya mazoezi.

"Kuanza utoaji wa huduma bado kidogo lakini hapa kila kitu kipo tayari bado vitu vidogo vidogo tu ili tuanze kupokea wagonjwa ambapo tunatarajia kutoa huduma kwa wananchi zaidi ya milioni moja kutoka seheme mbalimbali watakaokuja kupatiwa huduma "Alisema Mganga Mkuu Msanya.

Aidha aliongeza kuwa pindi hospital itakapoanza kutoa huduma itawasaidia wananchi wa Ubungo na sehemu zingine nyingi za karibu na hospital.

Naye Joseph Mtumwa  ambaye ni mwananchi aliyejitokeza kutoa Damu alisema kuwa hospital hii ilikuwa ikisubiliwa kwa hamu ili kusaidia upatikanaji wa huduma za tiba katika ambazo tulikuwa tukizifuata mbali kutokana na kutokukamilika kwa  hospital yetu.

Hivyo tunampongeza Diwani   kwa jinsi ambayo amekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa kata ya Kimara katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments