Na Shushu Joel,Pwani
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amewakumbusha wazazi na walezi wote katika Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanakuwa wasimamizi wakuu wa wanafunzi pindi wanapokuwa majumnbani na pindi wanapotoka shuleni kwa kusudi la kujua maendeleo yao kielimu.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akifafanua jambo kuhusu umuhimu wa kupeleka watoto shule mbele ya wazazi(NA SHUSHU JOEL)
Akizungumza
ofisini kwake Kunenge alisema kuwa wazazi na walezi walio wengi wamekuwa na
kasumba ya kutokufuatilia chochote kile iwe nyumbani wala shuleni kinachofanywa
na watoto wao hivyo hali hii ni hatari sana kwa kizazi cha kesho.
“Mzazi au
Mlezi ni wajibu wako kujua nini alichokifanya mtoto wako pindi anapokuwa
shuleni na hata anapokuwa nyumbani itamsaidia sana mwanafunzi kumjengea uwezo
wa kifkra mara kwa mara na kuwa mwepesi kuweza kuyakumbuka yale wanayoelekezwa
shuleni” Alisema Kunenge.
Aliongeza
kuwa ushirikiano baina ya wazazi,walezi na walimu utatengenezwa kizazi chenye
uwezo mkubwa katika Mkoa wetu na hivyo kuwa na vijana wengi watakao ongeza
nguvu kubwa katika serikali yetu kwa kipindi kijacho.
Aidha Kunenge alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imewekeza fedha nyingi katika miundombinu ya elimu kwenye Mkoa wa Pwani hivyo sasa Wazazi na walezi ni jukumu lao kuisaidia serikali kuhakikisha wanawasimamia wanafunzi ili kuweza kuwa na kizazi cha wasomi ambao watakaokuja kuja lulu kubwa katika Mkoa wetu wa Pwani.
Mbunge wa kibiti kushoto na mbunge wa Bagamoyo wakimfutialia kwa makini mkuu wa Mkoa wa Pwani
Mbali na
hilo Mkuu huyo wa Mkoa amewakumbusha walimu wote ndani ya Mkoa huo kutimiza
wajibu wao wa kuelimisha wanafunzi kwani elimu ni muhimu na wao ndio wategemewa
wakuu wa uelimisha wa wanafunzi wa ngazi zote.
Naye Ally
Hafidhi mmoja wa wazazi amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa kuwakumbusha wazazi na
walezi wajibu wao kitu ambacho wazazi na walezi wengi wamekuwa wakiwaachia
walimu tu kufanya majibu hayo.
Aidha
aliongeza kuwa kweli wazazi tumekuwa wazembe kuwauliza watoto wetu kile
walichokipata mashuleni kwa siku hiyo kutoka kwa walimu wao.
Kwa upande
wake Abiba Mitandi(49) alisema kuwa wazazi walio wengi wanajua jukumu la mzazi
ni kuhakikisha mwanafunzi anaendha shule tu lakini la kujua kasoma nini ni
suala ambalo linafanywa na walimu tu huko shuleni, sie kama wazazi au walezi
kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kujua mwanae kajifunza kipi huko shuleni na
hii ikifanyika sawasawa majumbani kwetun itaongeza tija kubwa sana katika Mkoa
wetu.
Aidha
amemsifu Mkuu wa Mkoa kwa maono yake ya mbali juu ya maendeleo ya Mkoa wetu wa
Pwani.
MWISHO
0 Comments