HOMOUD ABUU JUMAA APAMBANA NA MAJAMBAZI KUOKOA MAISHA YA MWANAMKE KARIAKOO

 Na Shushu Joel 

MBUNGE mstaafu wa Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoani Pwani Homoud Jumaa amefanikiwa kumuokoa  Mwanamke mmoja mkazi wa kariakoo jijini Dar es Salaam  mara baada ya kufyatua risasi kuelekeze kwenye hilo ghorofa ambalo Mwanamke huyo alikuwa akipiga kelele za kuomba msaada toka kwa raia wema mara baada ya kuvamiwa.

Homoud Abuu Jumaa aliyepambana kuokoa maisha ya Mwanamke jirani yake mara baada ya kuvamiwa na vijana wasiojulikana(NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza mara baada ya tukio hilo Jumaa alisema kuwa akiwa ndani kwake alisikia kelele zikipigwa ndani ya ghorofa hilo na kisha kutoka ili kujionea nini chanzo cha kelele hizo.

"Nilitoka nje na kuona watu wakimgasi gasi Mama huyo ndipo nilipoamua kupiga risasi ukutani kwenye ghorofa hiyo ya sita kwa lengo la kuwatisha vibaka hao" Alisema Jumaa

Aidha aliongeza kuwa nilitoka ndani kwangu na kukimbia kwenye tukio liliko ili kutoa msaada zaidi na kufanikisha kuingia ndani ya jengo hilo

Aliongeza kuwa nilifanikiwa kumsaidia Mwananmke huyo kwani hawakufanikiwa kuiba kitu chochote kile kutoka kwa Mwananmke huyo.

Kwa upande wake mmoja wa majirani wa maeneo hayo amempongeza Humud kwa ujasili wake aliouonyesha kwa kujitoa mhanga na kuingia ndani ili kutoa msaada zaidi.

" Jumaa ni mtu wa kuigwa sana katika jamii kwani wengi tuliongopa  na kujifungia ndani kwetu lakini kijana huyu alijitolea kumsaidia jirani yake kwa kweli Mungu ambariki sana shujaa huyu"Alisema.

Kwa upande wake Kamanda maalum ya Dar es Salaam Muliro Jumanne amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam huku akisema kuwa risasi tatu zilizo fyatuliwa hewani na vijana hao kukimbia hivyo kimsingi hakuna ujambazi uliofanyika katika eneo hilo.

Aidha Kamanda aliongeza kuwa uchunguzi unafanyika ili kujua vijana hao walikuwa ni akina nani na nia yao ni nini? Maana hawakuwa na bunduki wala panga.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments