Na Shushu Joel,Bagamoyo.
MWENYEKITI wa jumuiya ya wazazi(CCM) Mkoa wa Pwani Jackson Kituka amewataka wazazi wote wilaya ya Bagamoyo kusimamia maadili mema kwa watoto wao kama ilivyokuwa miaka ya zamani kwa upande wao walivyosimamiwa na wazazi hao.
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Pwani Jackson Kituka akisisitiza jambo mbele ya viongozi wa kata hawapo pichani(NA SHUSHU JOEL)
Rai hiyo
ameitoa alipokuwa akizungumza na viongozi wa jumuiya hiyo wilaya ya Bagamoyo
kwenye kikao maalum alichokifanya Mwenyekiti huyo ambacho kilikuwa na lengo la
kuimalisha jumuiya hiyo .
Aliongeza kuwa
watoto wetu wamekosa maadili mema tuliyofanikiwa kuyapata sie kipindi cha nyuma
hivyo kama wazazi ni lazima tukumbushane umuhimu wa kuwasimamia watoto wetu
ambao wameshindwa kuwa na maadili mema huku taifa likiwategemea kwenye masuala
mbalimbali.
“Sie tumebahatika kulelewa kwenye misingi ya kuwa na adabu na maadili ya hali ya juu lakini nashangazwa na kizazi cha sasa kuporomoka kwenye maadili huku watoto hao wakitokea kwenye majumba yetu”Alisema Mwenyekiti wa wazazi Mkoa huo wa Pwani Ndg Kituka.
Baadhi ya wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti wa wazazi Ndg Jackson Kituka
Kwa upande
wake Shabani Juma(67) mmoja wa wazazi waliohudhulia kikao hicho amempongeza
Mwenyekiti huyo kwa kutambua na kuona ni jinsi gani watoto wetu walivyoporomoka
kimaadili.
Aidha
amemwakikishia Mwenyekiti huyo kuwa kupitia nafasi yake ya uongozi ndani ya
jumuiya hiyo atahakikisha anatumua muda mwingi kuwakumbusha wazazi wengine
kuhakikisha wanawasimamia watoto kwenye misingi iliyo imara.
Naye Bi,Khadija Ally amempongeza Mwenyekiti huyo kwa maono yake ya mbali juu ya kuporomoka kwa maadili ya vijana wetu.
Pia amewakumbusha
wazazi kuwa na tabia ya kufuatilia mienendo ya watoto wetu kama ilivyokuwa
kipindi chetu ambacho wazazi wetu walikuwa wakitufuatilia kwa kila hatua ambayo
tulikuwa tukiipiga na ndio maana leo hii wengi wetu tumekuwa wazazi wa mifano
hivyo ni lazima kila mzazi awe makini na watoto wake na wa mwenzake kwa kusudi
la kurudisha maadili kwa vijana wetu
MWISHO
0 Comments