MUFTI AMTHIBITISHA SHARIFU KUWA BALOZI.

Na Shushu Joel

SHEIKH mkuu wa Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Muft Abubakar Zuberi amemthibitisha Alhaj Sharifu Zahoro kuwa Barozi wa dini ya kiislamu.

Mufti Abubakar Zuberi akifafanua jambo mbele ya waumini wa dini ya kiislamu juu ya umuhimu wa kusoma

Akizungumza na umati wa viongozi, waumini na wanafunzi wa dini ya kiislam katika hafla ya kuhitimu kwa wanafunzi wa Bakwata online Academy (TEHAMA)  Muft Zuberi alisema kuwa kazi ya ubalozi ni kubwa na yenye heshima kubwa katika dini yetu hivyo tumemkabidhi kazi hiyo Sharifu kutokana na utendaji wake wa kazi mbalimbali za kijamii.

“Awali nilitaka awe Balozi wa Mkoa wa Pwani lakini kutokana na utendaji wake kazi mbalimbali na tabia njema aliyonayo nimeamua awe balozi wan chi nzima kwani atakuwa msaada mkubwa katika Taifa letu”Alisema Muft Zuberi

Aidha alisema kuwa waislamu kila kikicha tunarudi nyuma kutokana na sababu za baadhi ya watu kuwa na tabia za wivu,ubinafsi, na ndio maana tumekuwa tukichelewa sana katika kufanya  maendeleo mbalimbali kwa kusudi la kulisaidia Taifa letu.

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa dini ya kiislam wakimpongeza Balozi Sharifu mara baada ya kuthibitishwa kuwa balozi na Muft Abubakar Zuberi

Kwa upande wake Balozi Sharifu Zahoro mara maana ya kuthibitihwa na Mufti Zuberi alisema kuwa kazi ya Mungu ni kujitolea hivyo nitahakikisha najitolea kwa moyo wangu wote ili tufike kule tunapopahitaji kufika.

Pia Balozi Sharifu amewasisitiza waumini wote wa dini ya kiislam na watanzania kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano kwake kwake bila wao hawezi kufanya kitu chochote chenye tija.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments