Na Shushu Joel
![]() |
Moja ya majengo ya shule yaliyojengwa na halmashauri ya Bukombe chini ya usimamizi wa Mkurugenzi Mtendaji George Lutengano(NA SHUSHU JOEL) |
MKURUGENZI mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe Mkoani Geita George Lutengano amefungua milango kwa watu mbalimbali kuweza kwenda katika halmashauri hiyo na kuwenza kujifunza namna jinsi wanavyofanikiwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kiwango cha hali ya juu.
Akizungumza
na waandishi wa habari Lutengano alisema kuwa Bukombe imekuwa ikitumia pesa
zote zinazoletwa na serikali kwa ajili
ya maendeleo ya wananchi kwa kufanya kile kilichokusudiwa kufanyika kwa
wananchi.
“Bukombe
imetekeleza miradi mbalimbali ambayo ilikuwa ni sugu na hata mingine mingi
mipya kwa kusudi la kuondoa changamoto kwa wananchi wetu ambao kipindi hiki cha
Rais Samia Suluhu Hassan wamekuwa na neema kubwa ya uwepo wa miradi mingi”
Alisema Lutengano.
Pia alisema
kuwa halmashauri ya Bukombe imefanikiwa kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo
shule za msingi na sekondari,miradi ya Afya,Nyumba za watumishi,Maji na
miundombinu vyote vikiwa ni utekelezaji wa wa serikali ya awamu ya sita chini
ya Rais Samia Suluhu Hassan
Naye Paul
Fumbuka mkazi wa Ushiromba amempongeza Mkurugenzi mteandaji wa halmashauri ya
Bukombe kwa jinsi ambavyo amekuwa mbunifu wa kuongeza mapato ya halmashauri na
vile ambavyo amekuwa akitekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ajili ya
wananchi wa halmashauri ya Bukombe.
“Sisi
wananchi wa Bukombe tunamshukuru sana Mhe: Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan
kwa kutuletea mkurugenzi mwenye uchu wa maendeleo kwa kuwaona wananchi wanakuwa
karibu na miradi muhimu kama vile Afya, miundombinu na miradi ya elimu” Alisema
Fumbuka.
Mwisho
0 Comments