WANAMICHEZO BUSEGA WAELEZA FAIDA ZA FEI CUP.

 Na Shushu Joel, Busega.

WANAMICHEZO mbalimbali katika wilaya ya Busega Mkoani Simiyu wameeleza namna ambavyo mashindano ya FEI CUP yanavyokwenda kuwanufaisha vijana.

Mkurugenzi wa mashindanio ya FEI CUP akifafanua jambo mbele ya mashabiki wa mpira wa miguu wilayani Busega(NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza na HABARI MPYA BLOG Mmoja wa wanamichezo wakongwe  katika kata ya Kiloleli Busweru Thomas alisema kuwa FEI CUP inakuwa kwa kasi na ni msaada kwa vijana wenye uwezo wa kusakata kandanda kuweza kufika mbali.

Aidha alisema kuwa fursa hizi zingetokea enzi zetu naamini tungefika mbali kwa vipaji tulivyokuwa navyo wakati tunacheza mpira.

" Mpira ni ajira kubwa sana katika ulimwengu wa sasa hivyo vijana onyesheni uwezo wenu ili mfikie malengo yenu" Alisema Busweru.

Naye mmoja wa vijana walionufaika na mashindano hiyo ambaye anathema katika timu ya Namungo alisema kuwa yeye bila FEI CUP angekuwa nyumbani tu huku ni mwenye kipaji cha ajabu.

Aidha amewataka vijana wenzake kutumia nafasi hiyo ili kutoka na kuitangaza wilaya yetu ya Busega.

Aidha mwandaaji wa mashindano hayo ya FEI CUP  Ndugu Feisal Almas mara baada ya kupigiwa alisema kuwa FEI CAP itaendelea daima.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments