RAIS SAMIA AKONGA MIOYO YA WANANCHI BUKOMBE: DC NKUMBA

Na Shushu Joel

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewakosha wananchi wa wilaya ya Bukombe Mkoani Geita kwa kuwashushia neema ya miradi mingi ya maendeleo kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Bukombe Said Nkumba 

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa wilaya ya Bukombe Said Nkumba alisema kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan imekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Bukombe kutokana na fedha nyingi za utekelezaji wa miradi.

“Bukombe tunamshukuru sana Rais Samia kwa utendaji wake wa kazi kwa kutushushia fedha za miradi kwa jamii na kutekeleja miradi yenye uhitaji mkubwa kwa wananchi”Alisema Nkumba

Aidha alisema kuwa wilaya ya Bukombe umepata fedha nyingi na imefanikiwa  kutekeleza ujenzi wa miradi kwa kiwango cha hali ya juu kutokana na usimamizi mzuri wa viongozi wa wilaya hiyo.

Aliongeza kuwa miradi iliyotekelezwa ni ujenzi wa shule,Nyumba za watumishi wa idara mbalimbali, Huduma za maji, Barabara na Taa za kisasa za barabarani kitu ambacho kinapelekea wilaya yetu kukosekana kwa usiku wala mchana kwani muda wote mji wetu unapendeza.

 

Kwa upande wake Bi, Maria Sololo (76) Mkazi wa Lunzewe alisema kuwa kwa kweli kipindi cha Rais Samia Suluhu Hassan maendeleo mengi yanafanyika ikilinganishwa na vipindi vingine hii ni kutokana na uchungu wa maendeleo alio nao Rais wetu Mhe. Samia kwa wananchi wake.

Aliongeza kuwa nimewaona marais wengi lakini Mhe. Samia amekuwa mkombozi mkubwa na hasa kwetu kina Mama kwani jinsi ambavyo hataki kutuona tukiangaika na masuala ya maendeleo ambayo yapo ndani ya uwezo wake.

“Awali tulikuwa hatujua ni kwnini Rais wetu anakwenda nje ya nchi kumbe ni kutuangaikia wananchi wake hivyo mimi namuombea Rais Samia apambane anavyojua ili wananchi wake tuneemeke kama anavyofanya sasa kwenye miradi mbalimbali”Alisema Bi, Maria

Aidha alisema kuwa kwa wilaya yetu ya Bukombe ni mengi yamefanyika chini ya Rais kipenzi Mhe.Samia Suluhu Hassan.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments