"MAONYESHO YA TATU YA UWEKEZAJI NA BIASHARA PWANI KUVUNA WAWEKEZAJI LUKUKI"RC KUNENGE

 Na Shushu Joel,Kibaha

MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema kuwa maonyesho ya tatu ya Uwekezaji na Biashara yanayokwenda kufanyika mwezi ujao katika viwanja vya mail moja vinakwenda kuleta mafanikio lukuki kutokana na jinsi ambavyo mipango inavyokwenda.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akifafanua jambo mble ya waandishi wa habari(NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza na HABARI MPYA BLOG Rc Kunenge alisema kuwa kufanyika kwa maonyesho hayo kunakwenda kuonyesha ulimwengu kuwa ni jinsi gani Mkoa wa Pwani ulivyo na mali ghafi za kutosha katika nyanja za uwekezaji.


Aidha alisema kuwa maonyesho haya ni fursa kubwa pia kwa wamiliki wa viwanda ambao tayari wamewekeza Pwani kwa kujitangaza na kujizolea wateja mbalimbali.


" Ni jambo la wazi Mkoa wetu unakwenda kuushangaza ulimwengu kutokana na kile ambacho kitafanyika katika maonyesho hayo" Alisema Kunenge 


Naye mmoja wa wawekezaji  ambaye amejitambulisha kwa jina la Le alisema kuwa Pwani ni sehemu sahihi ya uwekezaji wa nje kwani kila kitu kipo katika Mkoa wa Pwani.


Aidha tumpongeze Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha nia nzuri kwetu wawekezaji kitu ambacho kinakwenda kuifungia Tanzania.

Hivyo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge ni mtu mwenye maono ya mbali na maonyesho haya yanakwenda kuufungua Mkoa wa Pwani. 

MWISHO

Post a Comment

0 Comments