Na Shushu Joel, Kibaha
VIONGOZI mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wa Serikali wamempongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge kwa kuwa kiongozi wa pekee kwa ubunifu mkubwa wa kuweza kuvutia wawekezaji katika Mkoa huo.
![]() |
Naibu Waziri wa Ardhi Ridhiwani Kikwete akiwa na mkuu wa wilaya ya Kibaha(NA SHUSHU JOEL) |
Akitoa pongezi hizo kwa Kunenge Naibu Waziri wa Ardhi Ridhiwani Kikwete alisema kuwa Mkuu wa Mkoa amekuwa mtu sahihi katika shughuli mbalimbali za kuwaunganisha wananchi na serikali kwenye masuala mbalimbali ya kukuza uchumi wa wananchi mmoja mmoja na ongezeko kubwa la uwekezaji.
Aidha Kikwete aliongeza kuwa Rc Kunenge amekuwa msaada mkubwa kwa jamii ya Mkoa wa Pwani hasa katika utatutuzi wa changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa zimeshindikana kutatulika kwa kipindi kirefu.
" Leo Kunenge amefanikisha kuwakutanisha wananchi wa Pwani na wawekezaji mbalimbali wa viwanda kwa kusudi la kurahisisha huduma za uuzaji za mali ghafi za wananchi kwa wawekezaji" Alisema Kikwete
Pia Naibu Waziri huyo alitumia fursa ya uwepo wa maonyesho ya uwekezaji na Biashara kuwataka watumishi wa idara ya Ardhi kuhakikisha wawekezaji wanapewa hati za umiliki wa maeneo waliyoyawekeza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kibaha Mwajuma Nyamka amempongeza Mkuu wa Mkoa Kunenge kwa kuwa mbunifu mkubwa kwa ushawishi wake kwa wawekezaji.
Aidha aliongeza kuwa Chama Cha Mapinduzi kinatambua mchango wake mkubwa katika chama na hivyo kufanya wepesi wa utekelezaji wa ilani ya chama hicho.
Naye Juma Ally muuza juice ya mhogo alisema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge ni kiongozi asiye na makuu kwani kila sehemu amekuwa akifika na kutoa ushauri au maamuzi kwa lengo la kusaidia
MWISHO
0 Comments