Na Shushu Joel
Wadau wa Elimu kutoka katika Taasisi mbalimbali wamekutana jijini Dodoma kujadili rasimu ya maoni ya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na mabadiliko ya mitaala.
![]() |
| Naibu Waziri wa Elimu Kipanga akifafanua jambpo |
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda Jijini Dodoma amesema kuwa Mkutano utajikita katika kujadili rasimu ya Mapitio yaliyotoka na maoni mengi ya wadau yaliyokusanywa.
"Leo tuna Mkutano maalum, tunakutana kujadili Sera na Mitaala tukiwa na rasimu ni maelekezo ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akihutubia Bunge Mwezi Aprili 22, 2021 na katika majukwaa mbalimbali akiwa anatubia ameendelea kusisitiza hilo," amesema Waziri
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali kutoka Zanzibar Ali Abdulgullam Hussein ameeleze kuwa Sera na Mitaala ni nyenzo muhimu na msingi wa mafanikio ya elimu katika nchi yoyote Duniani na kuwataka wadau kushiriki kikamilifu katika kijadili rasimu hiyo.
"Sera madhubuti inatokana na maoni yetu wadau wote kwani kila mmoja ana mawazo yake na niwahakikishie kuwa mawazo yote ni muhimu, tutoe maoni ambayo yatapelekea kupatika sera na mitaala madhubuti kwa manufaa ya nchi" amesema Kiongozi huyo.
Wadau walioshiriki katika mkutano huo ni Wabunge Timu ya Zanzibar inayoshughulikia Sera na Mitaala, Vyuo Vikuu vya Umma na Binafsi, Taasisi za Umma na Binafsi, Taasisi za Dini, Bakita, Wadau wa Maendeleo na Wathibiti Ubora wa Shule


0 Comments