USHILIKISHWAJI WANANCHI SILAHA YA MAFANIKIO BUKOMBE: DED LUTENGANO

Na Shushu Joel

MKURUGENZI Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Ndg George Lutengano ameeleza kuwa siri ya mafanikio ya wilaya hiyo katika maendeleo ni ushilikishwaji wa wananchi mbalimbali katika wilaya hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe George Lutengano akifafanua jambo mbele ya wamabnu(NA SHUSHU JOE) 

Akizumgumza na waandishi wa habari Lutengano alisema kuwa wananchi wanaposhiliki kwenye mradi lazima mambo yaende vizuri kutokana na wananchi walio wengi kuhitaji maendeleo yaende kwa kasi hivyo wamekuwa wakijitolea mara kwa mara ili mkufanikisha miradi hiyo.

“Umoja tulionao wanabukombe ni wakuigwa sana kwani tumekuwa tukishirikiana kama mchwa nasi tumekuwa na umoja wa pekee kuanzia kwa wananchi mpaka kwa viongozi na ndio maana tumekuwa tukifanikiwa kwa nasilimia kubwa” Alisema Lutengano

Aidha Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa tumekuwa tukiwaeleza wananchi wetu uwazi kuwa serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan imekuwa ikifanya kazi usiku na mchana kwa kusudi la kufanikisha miradi ya maendeleo kwa wananchi wake hapa nchini.

Moja ya shule mpya zilizojengwa na halmashauri ya Bukombe ili kuwasaidia watoto waliokuwa wakitembea umbali mrefu(Na Shushu Joel)

Pia Lutengano amewakumbusha wananchi wa Bukombe kuendelea na moyo huo wa kujitolea kwenye masuala ya mafanikio yetu.

 

Naye Bi Tabitha Mabu ameipongeza serikali ya Bukombe kwa jinsi ambavyo imekuwa ikijitoa kwenye hamasa kitu ambacho kimepelekea kuwa na umoja wenye kujenga.

Aidha aliongeza kuwa tulichelewa sana miaka ya nyuma kwa kukosa umoja kitu ambacho sasa kipo na kinazidi kushirikiana.

MWISHO

 

Post a Comment

0 Comments