Na Shushu Joel, Bugombe.
MKUU wa wilaya ya bukombe Mkoani Geita Said Nkumba amewaeleza wananchi wa wilaya hiyo kuwa wilaya yetu itaendelea kupata miradi mingi na yenye uhitaji kutokana nan a malengo ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Shupavu Mhe: Samia Suluhu Hassan.
![]() |
Mkuu wa wilaya ya Bukombe Said Nkumba akizungumza na waandishi wa habari nofisini kwake. 9NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza ofisini kwake na waandishi wa habari Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ni msikivu na ni mpenda maendeleo kwa watu wake hivyo wana Bukombe tuendelee kumuombea Rais wetu ili aweze kufaniklisha ndoto zake za kuiona Tanzania ikiwa kwenye mabadiliko ya hali ya juu katika sekta mbalimbali za kimaendeleo.
Aidha
alisema kuwa mpaka sasa wilaya yetu ya Bukombe imepiga hatua kubwa katika
utekelezaji wa miradi ya maendeleo kitu ambacho hapo awali ilikuwa ni
changamoto kwa wananchi.
“Tuendelee
kumuombea Rais wetu ili aweze kuwa na Afya njema ili azidi kututumikia wananchi
wake wa Bukombe”Alisema Nkumba
Mpaka sasa
Rais Samia Suluhu Hassan kafanikisha uwepo wa
miradi mingi na yenye gharama kubwa
katika wilaya yetu ikiwemo Vituo vya Afya,shule za msingi na sekondari
katika maeneo ambayo yalikuwa hayana shule kabisa na zingine zilikuwa shule
shikizi,huduma za upatikanaji wa maji ya uhakika katika baadhi ya maeneo ya
wilaya yetu,miundombinu ya barabara kupitia wakala wa barabra vijijini na zile
za Tanroad hivyo uwepo wa vitu hivi vimepelekea kupatikana kwa maendeleo ya
haraka kwa wananchi wa Bukombe.
Juma Milanzi
ni mkazi wa Bukombe anasema kuwa kilichofanyika Bukombe kupitia Rais Samia
Suluhu Hassan ni hatua kubwa sana kwani ilikuwa tukiviona sehemu za mijini tu
lakini kwa sasa nasi tunavyo.
Aliongeza
kuwa Bukombe sasa tuna taa za barabarani kitu ambacho kimechangia kutokomeza
changamoto nyingi ikiwemo wizi na kuongeza thamani ya wilaya yetu ya Bukombe.
“Niwaombe
nwananchi wenzangu wa Bukombe kuendelea kumuombea Rais wetu Samia Suluhu Hassan
ili azidi kuiona Bukombe yetu katika maendeleo” Alisema
MWISHO
0 Comments