Na Shushu Joel,Pwani
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amezidi kuwa kinara katika ufanikishaji wa kila jambo ambalo amekuwa akiliofanya kwa jamii ya wakazi wa mkoa huo, kitu ambacho kimepelekea kuupaisha Mkoa huo katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akisistiza jambo .(NA SHUSHU JOEL) |
Kusudi la
Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani katika ufanisi mkubwa wa kubuni mambo mengi
yanayojkenga maendeleo ni kuwakutanisha wananchi na wazalishaji yaani wamiliki
wa viwanda na wakulima wa chini kabisa ambao wamekuwa wakililia upatikanaji wa
masoka ya kile wanachokizalisha,
Timu ya Blog
ya HABARI MPYA MEDIA imefanya utafiti mdogo
kwa jamii ili kujua ni sababu ipi
inayopelekea kila jambo linalosimamiwa na Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani Kunenge
limekuwa likifanikiwa kwa asilimia kubwa na kufanikiwa kupata baadhi ya maoni
ya wananchi mbalimbali juu ya suala la ufanisi unaofanywa na Kunenge.
Juma Hassan
ni mkazi wa Matipwili kata ya Mkange katika halmashauri ya Chalinze mara baada
ya kufanya mahojiano na mwandishi wa Makala hii alisema kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Pwani Alhaji Kunenge amekuwa akifanikiwa kutokana na kuwashirikisha jamii ya
watu wa chini na kuwauliza nini hitaji lao ambalo uenda lilikuwa sugu au la
sasa na wanataka lifanikiwaje hivyo katika mambo hayo Mkuu wetu wa Mkoa amekuwa
akifanikiwa sana.
Pia jambo
lingine ambalo limekuwa likimbeba Kunenge ni kubadikisha changamoto kuwa fursa
na hivyo baadhi ya wananchi wa hali ya chini kuzidi kunufaika na kile kilichopo
ndani ya Mkoa wao.
Aidha
tumuombe Mkuu wetu wa Mkoa azidi kutafuta wawekezaji wa viwanda kwani wamezidi
kuwa wakombozi wa suluhisho wa mambo mbalimbali ikiwemo ajira, uuzaji wa mali
ghafi kwa jamii zinzokuwa zimezunguka eneo hilo.
Kwa upande
wake Bi. Fatma Haji (65) mkazi wa kata ya Nia Njema wilaya ya Bagamoyo mara
baada ya kufanya mazungumzo na HABARI MPYA MEDIA alisema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani amekuwa
akifanikiwa vitu vingi kutokana na juhudi zake binafi anazowafanyia wananchi wa
Mkoa huo na hasa katika kusukuma
maendeleo.
“kwa kweli
tumefanikiwa kupata Mkuu wa Mkoa mwenye uchu mkubwa wa maendeleo tunaamini
Pwani tutafika mbali katika maendeleo”Alisema Bi, Fatma.
Aidha
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mamama Samia Suluhu Hassan
kwa jinsi ambavyo akiiangalia Pwani kwa jichio kubwa katika ufanisi wa miradi
ya maendeleo.
MWISHO

0 Comments