Na Shushu Joel, Mkuranaga
| Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega akiteta jambo na mwenyekiti wa CCM wilaya' |
MBUNGE wa jimbo la Mkuranga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mkoani Pwani Abdallah Ulega amezidi kutekeleza yale aliyoahidi kwa wananchi wa jimbo hilo bila wasiwasi wa aina yeyote ile.
Akizungumza kwenye Mkutano wa mwisho wa mwaka uliofanyika katika kata ya Mkuranga Naibu Waziri Ulega alisema kuwa ni mengi yamefanyika ndani ya kipindi hiki.
Aliongeza kuwa Mkuranga tangu inakuwa wilaya ilikuwa nyuma sana kwenye maendeleo ya sekta mbalimbali lakini kipindi ambacho nimekuwa Mbunge ni mengi yamefanyika na wananchi ndio mashaidi wakubwa.
" Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais kipenzi cha watanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan imekuwa msaada mkubwa kwenye utekelezaji wa miradi mingi ambayo ilikuwa ni historia ila sasa wananchi wa Mkuranga wananufaika nayo" Alisema Ulega.
Aidha Ulega amewataka wananchi kuendelea kuwa na subla kwani kuna mambo makubwa na mazuri yanakuja juu ya maendeleo kwa kuboresha na kuanzisha miradi ya kutosha ambayo itazidi kuiweka wilaya ya Mkuranga kwenye ramani kubwa ya kimaendeleo.
"Katika sekta ya Afya, Miundombinu,Umeme, Elimu na maji Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan imetupatia fedha za kutosho ambazo zinakwenda kutatua kero kubwa kwa wananchi wa Mkuranga" Alisema Ulega.
Aidha Ulega amewakumbusha wananchi kuendelea kutumia miradi hiyo kwa ufanisi kwa kuwa walinzi kwa watu wenye nia mbaya na miradi hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
Naye Hassan Mazengo mmoja wa Wananchi wa Mkuranga amempongeza Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo kwa jinsi ambavyo amezidi kuwa mkombozi kwa jamii.
"Tangu tunajitegemea kuwa wilaya hakuna kiongozi mahiri na aliyeibadilisha mkuranga katika sekta ya maendeleo" Alisema Mazengo.
Aidha Mazengo amemtaka Mhe. Ulega kuendelea na mwendo huo kwani wananchi tunamuelewa sana.
Naye Fatma Mkoga amemsifia Mhe. Ulega kwa jinsi ambavyo amekuwa kinara wa uletaji wa miradi ya Maji, Umeme, Miundombinu ya barabara na hivyo kupelekea kuwepo kwa muunganiko mkubwa wa maendeleo katika wilaya ya Mkuranga kitu ambacho awali ilikuwa ni histori.
MWISHO
0 Comments