Na Shushu Joel, Rufiji
ALIYEKUWA
Mwenyekiti wa kwanza wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania Hayati Bibi Titi Mohamed
amezidi kukumbukwa na jumiya hiyo kwa kuenzi yale aliyokuwa akiyafanya kwa
vitendo.
Wanawake
katika Mkoa wa Pwani wamekutana katika wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani kwa kusudi
la kuonyesha mapenzi yay a dhati kwa kuyafanya yale ambayo Bibi Titi alikuwa
akiyafanya kwa jamii yote ya watanzania.
Aidha aliongeza kuwa Wanawake tukiwa wamoja basi mambo mengi yatafanikiwa na hasa miradi mbalimbali.
“Nimpongeze
Rais Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo amekuwa nguzo ya Taifa hili kwa
jinsi ambavyo amekuwa akishusha maendeleo kwa watanzania.
Akizungumza
mara baada ya kikao kazi Mjumbe wa mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo na ambay pia ni
mbaraza Mariam Ulega alisema kuwa ni jambo la faraja kwetu Wanawake Mkoa wa
Pwani kwa kufanya maadhimisho ya kumbukumbu hayo katika Mkoa wetu.
Alisema kuwa
Bibi Titi amefanya mambo mengi katika Taifa hili ndio maana amekuwa akienziwa
kwa wema wake.
Naye
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo katika Mkoa wa Pwani Zaynabu Vulu amewasifia
Wanawake kwa jinsi ambavyo wamejitokeza katika maadhimisho hayo.
MWISHO
0 Comments