Na Shushu Joel, Kibaha
MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) kutokea Mkoa wa Pwani ( MBARAZA) Bi, Mariam Ulega ameahidi kutoa fedha ili kusaidia ujenzi wa nyumba za viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwezesha makazi bora kwa watumishi wa chama.
![]() |
Mjumbe wa Baraza la Taifa la UWT kutokea Mkoa wa Pwani Mariam Ulega akisisitiza jambo kwa wajumbe juu ya umuhimu wa kuwepo kwa nyumba za watumishi(NA SHUSHU JOEL) |
Ahadi hiyo ameitoa alipokuwa kwenye mkutano wa UWT walipokuwa wakiadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi(CCM) uliofanyika katika viwanja vya kwa Mbonde vilivyoko kibaha Mkoani Pwani.
Aliongeza kuwa Mimi kama mjumbe wa baraza nitatoa milioni mbili ili kuwezesha ujenzi wa watumishi ili watumishi wetu nao wajisikie vizuri katika utumishi wao wa Chama.
Aidha aliongeza kuwa uwepo wa nyumba za watumishi kutasaidia mambo mengi sana kwa watumishi wetu wa chama cha mapinduzi na hasa katika usalama wao.
Akisimamia zoezi hilo la uchangishaji wa fdha, vifaa na vitu mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi MNEC Hamoud Jumaa ambaye amesimamia zoezi hilo kwa ufanisi mkubwa na wa hali ya juu.
MWISHO
0 Comments