UWT KIBAHA VIJIJINI WAPANDA MITI KWENYE ENEO LA CCM.

 Na Shushu Joel, Kibaha.

Viongozi wa UWT wa Kibaha Vijijini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufyeka eneo lao(NA SHUSHU JOEL)

JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)  Wilaya ya kibaha vijijini Mkoani Pwani umepanda miti zaidi ya 1000 katika eneo la Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambalo linatarajiwa kujenga nyumza za watumishi wa chama hicho.

Wakizungumza mara baada ya kufyeka eneo hilo na kisha kupanda miti viongozi hao na Wanachama hao walikuwa na maoni mbalimbali ya kusema juu ya kutimia kwa miaka 46 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).


 Joyce Wasulwa ni mmoja wa wajumbe waliofanikiwa kufika kwenye eneo hilo na mara baada ya tukio hilo alisema kuwa ni jambo jema kuwa na eneo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba kwa ajili ya watumishi wa Chama na Jumuiya zake.


"Upanda huu wa miti unaashiria  uwekeaji safi wa mazingira yetu kwa ajili ya Taifa letu liwe la kijani na la kupendeza" Alisema.


Naye Katibu wa Jumuiya hiyo Bi, Nurath Ramadhani  alisema kuwa kupata kwa miti hii katika kiwanja cha Chama ni ishara kubwa ya maendeleo yanayozidi kufanywa na chama chetu.

Aidha alisema kuwa ni vyema kuendelea kuwa na umoja katika uongozi kwa kusudi la kuwasaidia wananchi wetu.

MWISHO


Post a Comment

0 Comments