MNEC JUMAA AONYA UKATAJI OVYO WA MITI NCHINI

 Na Shushu Joel,Kibaha 

MJUMBE wa halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (CCM) Hamoud Jumaa amewaonya watu wote wanaojihusisha na tabia ya ukataji ovyo wa miti katika maeneo yote ambayo uharifu huo umekuwa ukifanyika.

MNEC Hamoud Jumaa akisisitiza jambo juu ya umuhimu wa upandaji miti NA SHUSHU JOEL)


Rai hiyo ameitoa alipo kuwa  akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika  viwanja vya wazi vya picha ya ndege vilivyopo wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani. 


Aliongeza kuwa Taifa limeingia kwenye changamoto kubwa ya kimazingira kutokana na ukataji miti ambao umekuwa ukifanywa na binadamu kitu ambacho kimekuwa ma madhara makubwa ya kimazingira.


Aidha MNEC Jumaa amewataka wananchi kupanda miti kwa lengo la kuongeza uoto  wa asili ambao ulikuwepo kipindi cha Mababu zetu ambao waliona mbali kwa kupanda miti kila kona kwa lengo la kutunza mazingira.


" Nimeona sehemu nyingi watu wakipanda miti na hili ndio linatakiwa liwe ili kuongeza uoto wa asili wa mazingira kwani jua limekuwa kali na ukosekanaji wa kivuli umekuwa mkubwa hivyo pandeni miti ili tuweze kuwasaidia na viumbe hai vingine" Alisema MNEC Jumaa.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Bi Zaynabu Vulu amemsifu MNEC kwa uchapaji wake wa kazi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Pia amemwakikishia MNEC huyo kuwa jeshi la UWT litaendelea kumsemea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa yale anayoyafanya katika Taifa hili.


"Rais Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ametuheshimisha Wanawake wa Taifa kutokana na utekelezaji wake wa miradi mbalimbali mikubwa.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments