Na Shushu Joel, Kibaha
MWENYEKITI wa jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya kibaha vijijini Mkoani Pwani Bi, Leila Jumaa kwa kushirikiana na jumuiya hiyo wametembelea kituo cha watoto yatima kilichopo Mlandizi na kugawa zawadi mbalimbali kwa watoto hao.
Akizungumza alipokuwa akiwakabidhi vitu hivyo watoto hao Mwenyekiti huyo alisema kuwa wamefanya hivyo kama UWT kwa kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
" Watoto walio kwenye mazingira magumu ni watoto wetu sote hivyo jamii tunapaswa kuendelea kujitoa katika kuwasaidia misaada mbalimbali muhimu ili nao wajione jinsi gani wanapendwa nasi" Alisema Mwenyekiti huyo
Kwa upande wake Zuhura Mzava ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya wilaya amempongeza Mwenyekiti wa UWT wilaya hiyo kwa jinsi ambavyo amekuwa mstali wa mbele katika kuhamasisha jumuiya ya UWT kuweza kujitoa kwa jamii.
Aidha Mzava aliongeza kuwa ziara ya leo ya kwenda kwa watoto yatima ni funzo kubwa kwa jamii kwani kuna watu hawawezi kula mila mitatu kama ilivyo kwa watu wengine hivyo sasa ni vyema kuwa na moyo wa kujitolea kama ilivyoanzishwa na jumuiya yetu ya UWT hapa kibaha na wengine waige Mungu atawasaidia.
Naye Msimamizi wa kituo hicho amemponge Mwenyekiti wa UWT wilaya hiyo Bi, Leila Hamound Jumaa kwa kuona kituo hicho kinafaa kwa kupata misaada hiyo.
Pia ameongeza kuwa jambo hili limekuwa ni faraja kwetu pamoja na watoto kwa ujula wamefarijika sana.
MWISHO
0 Comments