WANACHUOI WAASWA KULINDA MZINGIRA

NA MWANDISHI WETU

 Wanafunzi wa vyuo nchini wametakiwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katikautekezaji wa shughuli mbalimbali za kuhifadhi na kulinda mazingira ilikupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba akifyeka 

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu waRais Dkt. Andrew Komba wakati akishiriki katika zoezi la usafi wa mazingirakatika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma lililoandaliwa na Jumuiya ya WanafunziTaasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) leo Januari 07, 2023.



Dkt. Komba ambaye amemwakilisha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais(Mazingira) Dkt. Switbert Mkama amesema kuwa zoezi hilo la usafi ni sehemu yakuungano mkono utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021.


Amewapongeza wanafunzi hao wa vyuo kwa kuandaa zoezi hilo la usafi ikiwa nikatika kuunga mkono juhudi za Serikali za usafi na uhifadhi wa mazingiraambapo kuanzia Januari 10, 2023 inatarajia kupanda miti katika Jiji la Dodoma.



“Kama mnavyofahamu Serikali ilishautenga Mji wa Dodoma kuwa wa mfanokatika masuala ya mazingira hivyo tunahakikisha tunapanda miti ya kutosha nanyie hapa leo mmeonesha mfano kwa kufanya usafi hospitalini hapa,” amesemaDkt. Komba.


Mkugenzi huyo ameongeza kuwa ni wakati muafaka kwa wanafunzi wa vyuokuwarithisha wadogo zao njia za kutunza mazingira kwa manufaa ya vizazi vyasasa na vijavyo.


Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Afya Mazingira Hospitali ya Mkoa waDodoma Paul Mageni amesema katika kuunga mkono Serikali wameanzishabustani ya miti katika eneo la hospitali hiyo.


Aidha, Mageni amesema miti iliyopandwa mbali ya kuhifadhi mazingira lakini piainawasaidia wananchi wanaopata huduma hospitalini hapo kupata hewa nzuri namatunda.


Kwa upande wao viongozi wa TAHLISO kutoka Tanzania Bara na Visiwani wametoa pongezi kwa uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma wa kuwapawasaa wa kufanya usafi katika eneo hilo.


Pia wamewapongeza wanafunzi wa vyuo mbalimbali walioshiriki katika zoezi hilo

ambalo ni njia mojawapo ya kuunga mkono Serikali katika kuhakikisha mazingira

yanakuwa endelevu kwa mustakabali wa taifa.

Post a Comment

0 Comments