Na Shushu Joel, Chalinze
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete amewahakikishia wananchi kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imedhamilia kutatua migogoro ya Ardhi kwa kiwango cha juu ili kuondokana na matatizo yanayowakqbili wananchi katika maeneo mbalimbali.
![]() |
Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza jambo mbele ya wadau ( NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo katika mwendelezo wa ziara zake Kikwete alisema kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametenga fedha kiasi cha shilingi Bilioni 345 kwa ajili ya kuhakikisha Ardhi inapangwa, inapimwa na inarasimishwa na wananchi wanapatiwa hati miliki ili kila mmoja aweze kutambua eneo lake linapoanzia na mwisho wake ili kuondoa mwingiliano wa mipaka ambayo imekuwa ikileta changamoto.
Aidha Kikwete alisema kuwa kupatiwa kwa fedha hizo na Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kumeleta neema kubwa kwa wizara yetu ya Ardhi kutokana na upimaji mkubwa unaenda kufanyika nchini kwa wananchi.
Hivyo Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Ridhiwani Kikwete amempongeza Rais Dkt Samia kwa jinsi gani ambavyo amekuwa msaada mkubwa kwa Taifa hili.
Naye Hawa Said Mkazi wa kata ya Mandela amempongeza Mbunge kwa jinsi ambavyo amekuwa kiongozi wa pekee katika utendaji wa shughuli za maendeleo za Jimbo na za kinchi.
Aidha amewataka wananchi kutumia nafasi hiyo ya upimaji wa Ardhi pindi utakapoanza waweze kutoa ushirikiano kwa watu wa wizara kwa lengo la kutatua changamoto hizo za migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza kwa jamii.
MWISHO
0 Comments