MLAWA AGAWA MADAWATI KUMALIZA CHANGAMOTO YA WANAFUNZI WANAOKAA CHINI BAGAMOYO.

 Na Shushu Joel, Bagamoyo 


Mwenyekiti wa Wazazi wilaya ya Bagamoyo Abubakari Mlawa katikati, Afisa Elimu wa Bagamoyo  kushoto,Mwalimu Mkuu Kiromo na Meneja wa Bank kushoto wakiwakabidhi wanafunzi madawati ( NA SHUSHU JOEL)

MWENYEKITI  wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania ( CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Ndugu Abubakari Mlawa amefanikisha ahadi yake ya kugawa madawati mia moja (100) katika shule ya msingi Kiromo kwa lengo la kuondoa changamoto iliyokuwa imedumu kwa muda mrefu sasa.


Akizungumza mara baada ya  kukabidhi madawati hayo Mlawa alisema kuwa Wazazi ni lazima kujitoljea ili kuweza kusaidia changamoto mbalimbali. 


Aidha alisema wanafunzi wanapokuwa wakisoma huku wakiwa wamekaa chini wanakuwa na uelewa ndogo kwa kuwaza namna jinsi wanavyopata elimu katika shule mbalimbali


"Tuendelee kuwasaidia wanafunzi ili waweze kukaa kwenye madawa na kuondokana na kero za kukaa chini na hii itawasaidia watoto wetu kuweza kuongeza uwezo wa ufaulu wa masomo yao" Alisema Mwenyekiti wa Wazazi Mlawa


Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kiromo Frola Mlowe amempongeza Mwenyekiti huyo wa Wazazi kwa kuona jinsi gani Kiromo inahitaji madawati hayo.


Aidha alisema kuwa anawaomba watu wengine waweze kujitoa kama Mlawa ambavyo amekuwa msaada kwa masula mbalimbali katika wilaya yetu ya Bagamoyo. 


"Mwenyekiti wetu wa Wazazi kwa niaba ya shule yetu ya Msingi Kiromo tunakumba undelete kutusaidia kwani bado uhitaji wetu ni mkubwa kwani bado tunahitaji madawati zaidi ya 200 lakini kwa haya 100 yanakwenda kupunguza changamoto ya ukaaji chini" Alisema  Mwalimu ........


Naye Meneja wa Stanibank tawi la Centre Richard Changa . ambao ndio wamefanikisha upatikanaji wa madawati hayo amesema kuwa Mwenyekiti wa Wazazi amekuwa akiomba misaada mbalimbali kwa kusaida jamii inayomzunguka ili iweze kuondokana na changamoto hizo.

Aidha alisema kuwa Bank yao itaendelea kutoa misaada hiyo kwa jamii ili kuiwezesha katika utatuzi wa mahitaji yao muhimu kutokana na jinsi tulivyojiwekea kama Bank

MWISHO

Post a Comment

0 Comments