DED CHALINZE KUMALIZA CHANGAMOTO YA KUKOSEKANA KWA MWALIMU MWANAMKE KWAIKONJE

 Na Shushu Joel, Chalinze.


MKURUGENZI Mtendaji wa halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Ndugu Ramadhani Poss ameahidi siku nne tu kumaliza changamoto ya kukosekana  kwa mwalimu wa jinsia ya kike katika shule ya Msingi Kwakonje iliyoko kata ya Miono.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Chalinze Ramadhani Poss akifafanua jambo mbele ya baraza la madiwani ( SHUSHU JOEL)

Akizungumza kwenye baraza la Madiwani Mkurugenzi Mtendaji alisema kuwa ni kweli kuna umuhimu sana wa kuwepo kwa Mwalimu huyo katika shule hiyo hivyo atahakikisha ndani ya siku hizo mwalimu anapatikana na kuweza kuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wa shule .


" Mwalimu wa Jinsia ya kike ni muhimu sana kuwepo katika shule yeyote ile hivyo  mimi kama mkurugenzi nafahamu umuhimu wake kwa watoto wetu wa kike" Alisema Poss


Aidha amewapongeza madiwani kwa jinsi ambavyo wamekuwa msaada mkubwa kwa kuibua changamoto zilizoko kwenye kata zao na kuzitatua na zile ambazo zimekuwa zikihitaji huduma ya Mkurugenzi nazi tunazitatua kwa haraka.


Kwa upande wake Diwani wa kata ya Miono Mhe. Juma Mpwimbwi amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Chalinze kwa jinsi ambavyo amekuwa mtendaji  wa haraka kwa changamoto ambazo tumekuwa tukimwakilishia.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments