UWT PWANI WATEKELEZA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS KWA VITENDO.

 Na Shushu Joel, Kibaha 

AGIZO lililotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Philip Isdor Mpango kwa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani limetekelezwa mara moja.

Mwenyekiti wa UWT Zaynabu Vulu na wabunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani wakionyesha ishara ya upendo (SHUSHU JOEL)

Akizungumza kwenye kikao cha kwanza cha Baraza la jumiuya hiyo Mwenyekiti wa UWT  Mkoa wa Pwani Bi Zaynabu Vulu amesema kuwa Jumuiya hiyo imezaliwa upya mara baada ya kukutana na kuamua kuvunja makundi yaliyokuwepo kipindi cha uchaguzi.


Mwenyekiti huyo alisema kuwa tumemaliza changamoto zilizokuwepo hapo awali na sasa Jumuiya yetu ya UWT inakwenda kuwa imara kama vile ilivyokusudiwa kufanyika.


Aidha amewataka Wanawake wote ndani ya Mkoa wa Pwani kila mmoja kwa wakati wake kujitengea nafasi ya kumsemea Mwanamke Mwenzetu ambaye amekuwa ni kinara wa utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. 


Aidha Bi, Vulu aliongeza kuwa ni vyema makundi  yamekwisha kwani ni aibu sana kwetu na chama kwa ujumla Hivyo kuisha kwake kunakwenda kufungua ufanisi mkubwa wa utendaji kazi za Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania katika Mkoa wa Pwani.


Naye Fatuma Mkoga ambaye alishida nafasi ya kuwa mjumbe wa kamati ya utekelezaji Mkoa alisema kuwa kushinda kwake kunakwenda kuongeza chachu ya ufanisi katika utendaji wa kazi za UWT  kutokana wajumbe wengi kuonekana ni vijana na wenye maono makubwa na jumuiya yetu.


Aidha aliongeza kuwa Mwenyekiti wetu Bi. Vulu  ni msaada mkubwa kwa UWT hivyo kila mmoja wetu ampe ushirikiano.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments