DIWANI PERA AMPA TANO KIKWETE.

 Na Shushu Joel  Chalinze.

DIWANI wa kata ya Pera, halamashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Ndugu Jackson Mkango amempongeza Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa jinsi ambavyo amekuwa mtekelezaji wa maendeleo katika kata hiyo.

Mbunge wa jimbo la chalinze ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na Diwani wa Pera Jackson Mkango

Akizungumza kwenye ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Diwani huyo alisema kuwa katika kata ya Pera kuna hatua kubwa ya maendeleo imefanyika na inazidi kufanyika kwa kasi kupitia Mbunge wa jimbo.


Aidha Diwani Mkango alisema kuwa tangu anaingia kwenye nafasi hiyo mwaka 2015 kwenye uchanguzi mkuu mpaka sasa kuna hatua kubwa zimefanyika kwenye Afya, Elimu, Umeme, Maji na miundombinu ikilinganishwa na vipindi vilivyopita.


Aidha Mkango amemuomba Mbunge kuendelea kushusha neema kwa kata hiyo kama anavyofanya sasa kwa wanqnchi hao ambao awali walikuwa na changamoto nyingi lakini sasa zinaendelea kutatulika kwa kasi kubwa.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Ridhiwani Kikwete amempongeza Diwani huyo kwa kuwa msimamizi mzuri wa miradi mikubwa inayotolewa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa wananchi mbalimbali. 


Aidha amewakumbusha wananchi kuwa ni vyema kuendelea kulinda miradi inayoletwa na serikali ili iweze kuendelea kutumika kwa kipindi kirefu.


Naye Sheikh Yusuph ( 82) amewapongeza viongozi hao kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakishirikiana kwa kuleta maendeleo katika kata ya Pera kitu ambacho miaka ya nyuma mambo yanayofanyika sasa  ni makubwa na yenye tija kwa wananchi.


Aidha amewataka Mbunge na Diwani kuendelea kushusha neema ya maendeleo kwa wananchi wa Pera ili waweze kujiwekea alama  kubwa kwa watu.


" Mhe Mbunge kamwambie Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa sisi cha kumlipa hakuna bali tutaendelea kumuombea Dua hili azidi kuwa nguzo kubwa ya maendeleo kwa Taifa hili" Alisema Sheikh Yusuph.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments