KIKWETE ATAKA WAZAWA WAPEWE KIPAUMBELE CHA AJIRA KWENYE MIRADI.

 Na Shushu Joel, Chalinze.

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete amewakumbusha watumishi wote wa serikali kuhakikisha wanawapatia kipaumbele wananchi ambao wanazungukwa na mazingira ambayo miradi ya serikali inajengwa

Naibu Waziri wa Ardhi akitoa ufafanuzi juu ya wakandarasi kutoa ajira kwa watu wanaozunguka miradi.( SHUSHU JOEL)

Hayo ameyasema alipokuwa akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Magome kata ya Pera,halamashauri ya Chalinze katika mwendelezo wa vikao vyake vya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Jimbo hilo.


Naibu Waziri Kikwete alisema kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imekuwa na makusudi makubwa kwa wananchi na ndio maana amekuwa akitekeleza miradi ya maendeleo ya kutosha ili kuwaondolea wananchi changamoto za maendeleo ambazo zimekuwa zikiwakabili watanzanzia.


Aidha alisema kuwa ujenzi huu wa mradi wa Julias Nyerere Hadro Power project (kituo cha kupozea umeme Chalinze) ni muhimu wananchi wa chalinze wakapata ajira kutokana na uwepo wa kituo hicho.


Kwa upande wake Mwakilishia wa Tanesco  Elieza  Minja alisema kuwa wapo baadhi ya wananchi waliopata ajira kwenye mradi sema tu kuna mambo ambayo serikali imeyaandaa kwa wananchi kwani bajeti ijayo inaenda kumaliza tatizo hilo kwa wananchi wa Pera.


Aidha amemwakikishia Naibu Waziri wa Ardhi kuwa  ajira zinaenda kupatikana muda si mrefu na zitaenda kuwapa neema wananchi hao.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments